Wednesday, July 08, 2015

RAIS KIKWETE ATUA DODOMA, KUTEGUA KITENDAWILI CHA NANI MTEULE WA CCM KUWANIA URAIS WA TANZANIA WIKI HII

RAIS KIKWETE ATUA DODOMA, KUTEGUA KITENDAWILI CHA NANI MTEULE WA CCM KUWANIA URAIS WA TANZANIA WIKI HII
 MWENYEKITI wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, akiongozana na Katibu Mkuu wa chama hicho, Abdulrahman Kinana, (kulia), akiwapungia wana CCM waliofika kumlaki kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma Julai 8, 2015. 

Mwenyekiti huyo wa CCM amewasili na kuanza kazi mara moja ya kuongoza kikao cha kamati ya maadili ili kupokea taarifa za watia nia wa CCM, kabla ya kuanza kuwajadili na kupunguza majina kutoka 39 hadi matano, kazi itakayofanywa na Kamati Kuu ya chama hicho inayotarajiwa kukutana Alhamisi Julai 9, 2015 majira ya usiku. 

Baada ya zoezi hilo la Kamati Kuu, majina hayo matano yatapelekwa kwenye Halmashauti Kuu ya CCM, nayo itakaa na kuyapunguza tena na kufikia majina matatu ambayo nayo yatapelekwa mbele hya wajumbe zaidi ya 2000 wa Mkutano Mkuu wa chama hicho hapo Julai 12 na kuchaguz jina moja ambalo ndilo litapitishwa nan kuwa mgombea wa CCM wa kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015
MWENYEKITI wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, akiongozana na Katibu Mkuu wa chama hicho, Abdulrahman Kinana, (kulia), akiwapungia wana CCM waliofika kumlaki kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma Julai 8, 2015. 
 Rais Kikwete, akisalimiana na viongozi wa juu wa chama hicho, makamu mwenyekiti (Bara), Philip Mangula, Katibu Mkuu, Abdulrahmani Kinana, Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye