Tuesday, July 14, 2015

KAMBI YA JESHI YAPOROMOKA NA KUUA 23 URUSI



KAMBI YA JESHI YAPOROMOKA NA KUUA 23 URUSI
Kambi ya jeshi yaporomoka na kuua 23 Urusi
Takriban wanajeshi 23 wa Urusi wameuawa karibu na mji wa Omsk ulioko Siberia baada ya jengo la kambi ya kijeshi kuporomoka.


Wanajeshi wengine 19 waliokolewa kutoka kwa vifusi vya jengo hilo.
Mwanajeshi mmoja aliyeokolewa ameileza runinga ya Urusi kwamba wanajeshi walikuwa wamelala wakati wa ajali hiyo.
Picha za televisheni zilionyesha sehemu ya jengo hilo la ghorofa nne likiwa limeharibika kabisa huku wanajeshi wakishirikiana kuondosha vifusi.
Mwandishi wa BBC Moscow amesema inadhaniwa kwamba ukarabati duni uliofanyika mwaka jana ndio uliosababisha kuporomoka kwa jengo hilo.