Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa Taasisi ya Maendeleo ya Elimu Mkoa wa Morogoro (MEDO), James Mbuligwe (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, kabla ya MC Pilipili kutiliana saini na taasisi hiyo ya kusaidia elimu. Kutoka kulia ni Meneja Mradi, Bertha Gama, Emmanuel Elias 'MC' Pilipili na Makamu Mwenyekiti wa Medo, Seluwa Amin.
MC Pilipili (katikati), akizungumza kabla ya kutia saini.
Makamu Mwenyekiti wa Medo, Seluwa Amin (kushoto), akiangalia mkataba huo kabla ya kusainiwa.
MC Pili pili (katikati), akisaini mkataba huo.
Makamu Mwenyekiti wa Medo, Seluwa Amin (kushoto), akimkabidhi mkataba huo MC Pilipili. Kulia ni Meneja Mradi Medo, Bertha Gama.Na Dotto Mwaibale
MSANII na mshereheshaji wa shughuli mbali mbali, Emmanuel Elias 'MC' Pili pili ameingia mkataba na Taasisi ya Maendeleo ya Elimu Mkoa wa Morogoro (Medo), kwa ajili ya kusaidia elimu.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana kabla ya kusaini mkataba wa kusaidia watoto walio katika mradi wa elimu kwa watoto unaoendeshwa na Medo, Pilipili alisema ni wakati muafaka kwa watanzania kwa ujumla kujenga tabia ya kusaidia shughuli za maendeleo hasa katika elimu.
Alisema bila ya kuwa na elimu hakuna kinachoweza kufanyika katika mambo mbalimbali pamoja na uongozi hivyo kila mtu eneo alipo anapaswa kusaidia elimu kupitia taasisi hiyo ya Medo ili iweze kuwasaidia watoto wengi zaidi.
"Napenda kuwasapoti watoto hawa waliochini ya mradi unaoendeshwa na Medo kwa kuwasaidia mahitaji mbalimbali hivyo naomba watanzania wanisapoti wakiwemaniio wasanii wenzangu" alisema Pilipili.
Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa Taasisi ya Maendeleo ya Elimu Mkoa wa Morogoro, James Mbuligwe alisema taasisi yake kuingia mkataba na MC Pili pili kwa ajili ya kuwasaidia watoto hao ni hatua nzuri ya mafanikio kwao.
Alisema taasisi hiyo imezindua kampeni maalumu ya 'Nisaidie 500 Yatosha kunipa elimu ambapo balozi wa mradi huo ni Msanii Wastara Sajuki" alisema Mbuligwe.
Meneja wa Mradi huo, Bertha Gama alisema hadi hivi sasa kuna watoto 35 wanaopata elimu ya Sekondari katika shule za Kauzeni, Kihonda, Mwembesongwe na Mzinga na kuwa mwaka huu wanafunzi wanne waliochini ya mradi huo wanategemewa kuhitimu kidato cha nne.
Alisema lengo la taasisi hiyo ni kufikisha huduma zao nchi nzima ambapo kwa awamu ya kwanza wameanzia mkoani Morogoro na kupitia chini ya mradi huo watoto 100 watanufaika na kwa awamu ya pili wanatarajia kuifanya mikoa ya Kanda ya Ziwa. (Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)