Makongoro Nyerere wakati wa zoezi la kutangaza nia jana.
Makongoro Nyerere baada ya kuvishwa vazi aina ya mgolole.
Makongoro akifanyiwa maombi wakati wa kutangaza nia.
MBUNGE wa Bunge la Afrika Mashariki, Charles Makongoro Nyerere, hatimaye jana naye ametangaza nia yake ya kuwania Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Makongoro alitangaza nia yake huko Mwitongo mita chache kutoka kaburi la Baba wa Taifa, Mwl. Nyerere wilayani Butiama mkoani Mara.
Katika tukio hilo, Makongoro aliwalaumu baadhi ya viongozi wakuu wa serikali kutumia nafasi zao serikalini hivi sasa kuwatisha wakurugenzi wa majiji, manispaa na halmashauri za wilaya kwa kutaka kupewa fedha za kuwawezesha kugombea nafasi ya Urais huku wakifikia hatua ya kufukuza wakurugenzi kazi wanaoshindwa kutii maagizo hayo.
Aidha kuhusu suala la rushwa nchini, Makongoro alisema CCM imekithiri kwa rushwa na kusababisha tatizo ambalo limesambaa kwa taifa zima hata kuwanyima haki baadhi ya watu na kusabisha chama hicho kuwa na makundi makubwa yanayotishia amani hivyo kuomba ridhaa ya kuwania Urais ili kurejesha chama hicho kwa wanachama.
Makongoro alikataa kuzungumzia ajenda zake za mipango ya maendeleo kwa Tanzania hivi sasa kwa maelezo kuwa chama hicho kina taratibu zake kwa kufuata ilani ya CCM inayotarajia kupitishwa mwezi Julai mwaka huu.