Thursday, May 14, 2015

MTOTO WA BABA WA TAIFA AZIKWA BUTIAMA



MTOTO WA BABA WA TAIFA AZIKWA BUTIAMA
 Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Musoma Mhashamu Michael Msonganzila akisali mbele ya jeneza la marehemu John Guido Nyerere kabla halijaingia kanisani kwa ajili ya ibada maalum iliyofanyika kwenye Kanisa Katoliki la Bikira Maria wa Damu Azizi ya Yesu Jimbo la Musoma Parokia ya Butiama.


 Viongozi na wananchi wakishiriki ibada ya kumuombea marehemu John Gaudo Nyerere katika Kanisa Katoliki la Bikira Maria wa Damu Azizi ya Yesu Jimbo la Musoma Parokia ya Butiama
 Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Musoma Mhashamu Michael Msonganzila
akitoa heshima za mwisho kwa marehemu John Guido Nyerere baada ya kukamilika kwa ibada maalum iliyofanyika kwenye Kanisa Katoliki
la Bikira Maria wa Damu Azizi ya Yesu Jimbo la Musoma Parokia ya
Butiama.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye akizungumza na Mbunge wa Jimbo la Monduli na Waziri Mkuu Mstaafu Ndugu Edward Lowassa wakati wa mazishi ya John Guido Nyerere yaliyofanyika nyumbani kwa Baba wa Taifa ,Butiama.
 Jeneza lenye mwili wa marehemu John Guido Nyerere likiteremshwa kaburini na Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
 Mama Maria Nyerere akiweka udongo kwenye kaburi la mtoto wake John Guido Nyerere.
 Waziri wa Katiba na Sheria Dk. Asha-Rose Migiro akiweka udongo kwenye kaburi la John Guido Nyerere.
 Mtoto wa mwisho wa marehemu John Guido Nyerere anayefahamika kwa jina la Wanzagi akilia kwa uchungu huku akifarijiwa na shangazi yake Anna Nyerere.
 Ni huzuni kwa kila mtu.
 Mama Maria Nyerere akiweka shada la mau kwenye kaburi la mtoto wake John Guido Nyerere.
 Mtoto wa Marehemu anayeishi Lusaka Zambia, Sofia Nyerere Mwape akiweka shada la maua kwenye kaburi la Baba yake marehemu John Nyerere.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akitoa heshima mbele ya kaburi la marehemu John Gaudo Nyerere mara baada ya kuweka taji la maua.
 Mbunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki Shyrose Bhanji akiweka shada la maua kwenye kaburi la marehemu John Nyerere kwenye mazishi yaliofanyika nyumbani kwa marehemu Baba wa Taifa Butiama.
Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakishiriki kuweka mashada ya maua kwenye kaburi la John Guido Nyerere.
 Baadhi ya Watoto wa marehemu pamoja na ndugu wengine.
 Mheshimiwa Waziri wa Katiba na Sheria Dk. Asha-Rose Migiro akisoma salaam za rambi rambi kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri wa Muungano wakati wa mazishi ya John Nyerere.
Emily Magige Nyerere akifafanua jambo wakati wa mazishi ya John Guido Nyerere.
(Picha zote na Adam H. Mzee)