ASKARI wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) Kambi ya Lugalo, Barnabas Mataja (48), amefariki dunia baada kusombwa na maji katika Mto Mzinga.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, ACP Japhari Mohamedi, alisema tukio hilo lilitokea Mei 11, mwaka huu katika eneo la Kimbangulile, Kata ya Tambani, Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani.
Mohamedi alisema marehemu alikuwa akirudi nyumbani kwake akitokea matembezini, wakati akivuka mto huo maji yalimzidi nguvu na kumsomba.
"Mwili wa marehemu umepatikana Mei 12, mwaka huu saa nne asubuhi katika eneo la Tambani," alisema Kamanda Mohamedi.