Wednesday, April 15, 2015

WALIOFARIKI KWA RADI MKOANI KIGOMA WAAGWA



WALIOFARIKI KWA RADI MKOANI KIGOMA WAAGWA
Miili ya wanafunzi sita, Mwalimu mmoja na mkazi wa eneo la Bangwe ikiwa tayari kwa kuagwa katika viwanja vya shule ya Msingi Kibirizi mkoani Kigoma.


Wanajeshi wa JWTZ wakiingiza miili ya marehemu katika viwanja vya shule ya msingi Kibirizi kwa ajili ya kutoa heshima za mwisho.
Watu wanane wakiwemo wanafunzi sita wa shule ya msingi Kibirizi, mwalimu mmoja pamoja mkazi wa eneo la Bangwe mjini hapo walipoteza maisha hapo jana baada ya kupigwa na radi huku wanafunzi wengine 15 wakijeruhiwa na radi hiyo.
Miili ya marehemu imeagwa mchana huu wa leo katika viwanja vya Shule ya Msingi kibirizi tayari kwa mazishi.
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Kanali Mstaafu Issa Machibya alihudhuria katika shughuli hiyo ya kuwaaga marehemu wanjani hapo na kutoa salamu za rambi rambi kwa ndugu na jamaa za wafiwa.
kwa upande wake, Katibu wa Bakwata mkoa wa Kigoma, Shekhe Moshi Guoguo alitoa salamu za rambirambi kwa wafiwa na Taifa kwa ujumla, aliwataka waombolezaji kuwa wapole na wavumilivu hasa katika wakati huu mgumu wa majonzi ya kupotelewa na ndugu zao wapendwa.
BWANA ALITOA, BWANA AMETWAA. JINA LA BWANA LIHIMIDIWE!
CHANZO: MICHUZI BLOG