Wakulima wa Mpunga na mahindi wilayani Movemoro Mkoani Morogoro wameitaka serikali kuwafikishia kwa wakati mbolea na pembejeo za kilimo ili waweze kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.
Wamesema mara kwa mara mbolea na pembejeo za ruzuku zimekuwa zikifika kwa kuchelewa wakati msimu wa kupanda au kuweka mbolea ukiwa umekwisha na wakati mwingine kukaa kwa muda mrefu ghalani na wakulima kupewa ikiwa tayari imeharibika.