Saturday, April 04, 2015

Wakazi 300 wakosa mahali pakuishi baada ya nyumba zao kusombwa na maji ya mvua iliyonyesha mkoani Simiyu.


Wakazi 300 wakosa mahali pakuishi baada ya nyumba zao kusombwa na maji ya mvua iliyonyesha mkoani Simiyu.
Watu 300 wakazi wa kijiji cha lamadi wilayani Busega mkoani Simiyu hawana mahali pa kuishi kutokana na nyumba zao kusombwa na maji kutokana na mvua kubwa iliyonyesha kijijini hapo usiku wa kuamkia leo.
Vitongoji vilivyokubwa na mafuriko hayo ni kisesa,sokoni mwalukonge,lukungu,iseni b na mwabayanda ambapo nyumba 200  zimesombwa na maji.
 
Wakiongea na ITV wananchi hao wamesema kuwa walikumbwa na mafuriko hayo majira ya saa sita usiku ambapo maji yalijaa katika nyumba zao na kusomba vitu mbalimbali pamoja na kuku hali iliyowalazimu kukimbilia katika shule ya msingi nyamajashi kwa ajili ya kujihifadhi.
 
Diwani wa kata ya lamadi,Emanuel Desera amesema hali za wananchi hao kwa hivi sasa siyo nzuri na kwamba wengine wamekimbilia kwa ndugu zao kujihifadhi na kwamba hali ya mafuriko bado inaongezeka ambapo ameiomba serikali kupeleka msaada wa chakula madawa na mahema kwa wahanga hao.
 
Baadhi ya viongozi mbalimbali ikiwemo kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo ikiongozwa na mkuu wa polisi wa wilaya hiyo iko katika eneo la tukio kwa ajili ya kuangalia usalama wa wananchi hao waliokumbwa na mafuriko.