Tuesday, April 07, 2015

Tishio la Ugaidi: Waziri Wa Mambo Ya Ndani Asema Nchi Ipo Katika Hali Ya Tahadhari



Tishio la Ugaidi: Waziri Wa Mambo Ya Ndani Asema Nchi Ipo Katika Hali Ya Tahadhari

Waziri wa Mambo ya ndani  ya  Nchi,Matthais Chikawe amesema nchi  ipo katika tahadhari ya juu  kufuatia taarifa za vyombo  mbalimbali  vya habari  kwamba, kuna uwezekano wa shambilio la ugaidi katika miji ya Dar es salaam na Mwanza.
 
Chikawe amesema hayo ikiwa  ni  siku  chache  baada  ya  taarifa  kusambaa kuwa mmoja ya waliokamatwa katika shambulio la chuo kikuu cha Garissa nchini Kenya ni Mtanzania.
 
Akiongea  na  BBC, Chikawe  amesema mpaka sasa serikali bado haijaweza kuthibitisha ripoti hizo  lakini vyombo vya dola nchi nzima viko macho na vimejitayarisha kwa lolote.
 
Pamoja na hayo waziri Chikawe amesema kuwa serikali inafahamu kuwa mmoja ya watuhumiwa walikokamatwa huko Garissa Kenya ni Mtanzania.
 
Hata hivyo amesema watawasiliana na polisi wa Kenya wakimaliza kumhoji mtuhumiwa huyo.