Thursday, April 09, 2015

Mwanajeshi wa JWTZ Ajinyonga Jijini Mwanza



Mwanajeshi wa JWTZ Ajinyonga Jijini Mwanza  

Fundi wa magari wa Kikosi cha Jeshi la Ulinzi la Wananchi namba 512 MTC Nyegezi, jijini Mwanza, Jacob Mponeja (55) amekutwa amejinyonga chumbani kwake kwa kutumia kamba ya katani huku akiacha ujumbe.

Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, Joseph Lusungu tukio hilo lilitokea Aprili mosi mwaka huu majira ya saa moja asubuhi.
Alisema ujumbe huo ulioandikwa kwenye kitabu kidogo kilichokutwa kwenye eneo la tukio ulisomeka; "Kifo changu kimetokana na mke wangu kujihusisha na vitendo vya kishirikina, hali iliyosababisha kutaka kuuawa mara mbili na mtu asilaumiwe kwa kifo changu."
Alisema kwa mujibu wa mtoto wa marehemu, ambaye ni mwanafunzi katika sekondari ya Nyabulogoya, kabla ya tukio la kujinyonga, baba na mama yake Happy Mabula (45), walikuwa na ugomvi mkubwa.
Kaimu Kamanda huyo alisema katika ugomvi huo mama huyo alikatwa shoka na mumewe na kwamba alikimbizwa katika hospitali ya Rufaa ya Bugando kwa matibabu na kwamba hali yake sio nzuri.
Alisema katika eneo la tukio kulikutwa shoka lililokuwa na damu pamoja na kitabu hicho kidogo kilichokuwa na ujumbe ulioandikwa na marehemu.
------------
Mechanic of the Defence Force Army Men MTC Nyegezi numbers 512, Mwanza, Jacob Mponeja (55) has found he hanged himself in his room with a hemp rope as he left a message.
 
According to Acting Regional Police Commander of Mwanza, Joseph Lusungu the incident occurred Saturday in April this year at one summer morning.
 
He said the message was written on a little book kilichokutwa on the scene was readable, "my death has been driven by my wife engaging in superstitious practices, state effected wanting to be killed twice and one should be blamed for my death."
 
He said according to the child of the deceased, who is a student at the secondary Nyabulogoya, prior to the occurrence of suicide, his father and mother Happy Mabula (45), had a greater variance.
 
Acting Commander said in the same variance axes woman beheaded her husband and that he rushed into the Bugando Referral Hospital for treatment and that his condition is not good.
 
He said at the scene were found to ax sprinkled with blood with the little book was a message written by the deceased.