Saturday, April 04, 2015

MUIGAZAJI WA FILAMU AHAMA KISA USHIRIKINA



MUIGAZAJI WA FILAMU AHAMA KISA USHIRIKINA Tiko Hassan ameikimbia nyumba aliyokuwa akiishi maeneo ya Mwananyamala jijini Dar kutokana na mambo ya kishirikina.Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni Tiko alisema kuwa, ameamua kuihama nyumba hiyo licha ya kwamba kodi yake haijaisha kufuatia maruweruwe yaliyokuwa yakimpata nyakati za usiku.
Mwanadada kutoka tasnia ya filamu na muziki Bongo, Tiko Hassan.
"Yaani nimekuwa nikishindwa kulala kwa raha kwani usiku huwa nasikia sauti za ajabu, mara nahisi kuna watu wanatembea ndani, mara mapaka yanalia dirishani kwangu, kimsingi sikuwa nikiishi kwa amani, nimeona nihamie Kinondoni yasije yakanikuta makubwa," alisema Tiko.