Sunday, April 05, 2015

mmoja wa Al Shabaab aliyeuwawa na polisi katika mapambano ya chuo garissa ni msomi mwenye Shahada ya uwakili alifuzu katika Chuo Kikuu cha Nairobi



mmoja wa Al Shabaab aliyeuwawa na polisi katika mapambano ya chuo garissa ni msomi mwenye Shahada ya uwakili alifuzu katika Chuo Kikuu cha Nairobi
Al Shabaab wanasajili vijana wasomi kama AbdiRahim Abdullahi aliyekuwa na Shahada ya uwakili na aliyeuawa katika shambulizi la Garissa. Idara ya polisi nchini Kenya inasajili wanafunzi waliopata alama ya D+ katika mtihani wa KCSE.

Abdirahim Abdullahi ni mmoja ya Al Shabaab waliyouawa baada ya kuuwa zaidi ya Wakenya 147.
Abdirahim ni wakili na alifuzu na shahada ya uwakili kutoka Chuo Kikuu cha Nairobi mnamo mwaka 2013. Wanaomjua wamemtaja kuwa wakili stadi.
Alisomea shule ya upili ya WAMY jijini Nairobi na kufuzu na alama ya A-. Wanaomjua kijana huyu wamemtaja kuwa kijana mahiri na msomi.
Ni mtoto wa chifu mmoja mjini Mandera. Inasemekana alitoweka kwao mwaka mmoja uliopita. Kitendo alichokitekeleza cha mauaji ya wanafunzi Garissa kimemsikitisha sana babake mzazi.

Je, hii inachangia katika hali ya vikosi vya usalama vya serikali ya kenya kushindwa hekima wa magaidi?
vipi je elimu ya polisi wa tanzania?