Mamia ya wahamiaji wanahofiwa kufa maji baada ya boti iliokuwa wakiabiri kuzama karibu na pwani ya Libya.
Shirika la Umoja wa mataifa linataja ajali hiyo kama mbaya zaidi katika bahari ya sham.
Operesheni kubwa inaendelea katika kisiwa kilichoko Kusini mwa Italia cha Lampedusa mahali ambapo inaaminika zaidi ya wahamiaji 700 wamekufa maji.
Wahamiaji hao wanaaminika walikuwa wakivuka bahari kukimbilia bara Ulaya.
Chombo hicho cha majini kinaaminika kilikuwa kikiwabeba wahamiaji hao mia saba kutoka kazkazini mwa Afrika.
Duru za hivi punde zasema kuwa wahamiaji 28 pekee ndio wamefaulu kuokolewa kufikia sasa.
Meli ishirini za kijeshi na ndege za Helikopta zinashiriki katika shughuli za uokoaji.
Inaaminika kuwa ajali hiyo ilifanyika katika maeneo ya bahari nchini Libya kilomita 200 kusini mwa Lampedusa.
Ni kisa cha hivi punde cha misururu ya kuzama kwa maboti yanayowabeba wahamiaji.
Juma lililopita, watu mia nne walifariki huku boti jingine likizama kazkazini mwa Libya ndani ya bahari ya Sham.