Wasichana 22 walioingizwa nchini na mmiliki wa Continental Night Club , Omprakash Singh kwa ajili ya kufanya biashara ya ukahaba wamerudishwa kwao Nepal na India walikotoka.
Kamishna wa Uhamiaji Udhibiti na Usimamizi wa Mipaka, Abdallah Abdullah, alisema wasichana hao waliondoka jana baada ya kumaliza matibabu waliyokuwa wakipata. "Wasichana waliokuwa wanaugua TB na UTI wote wamepona, tiketi zilichelewa kidogo lakini imepatikana,"alisema.
Alisema Singh ameshalipa faini ya Sh milioni 15 alizoamuliwa kulipa na mahakama, pamoja na kulipa mishahara ya wasichana hao Dola za Marekani 30,625. Tangu wasichana hao walipobainika walikokuwa wamefichwa, Idara ya Uhamiaji imekuwa ikiwasimamia kwa kuwapa matibabu na kufanikisha safari ya kurudi nchini mwao.
Unadhani nini kinasabisha wamiliki wa sehemu za burudani kuagiza makahaba kutoka India?