Baadhi ya wagonjwa mkoani Kilimanjaro wameishangaa Hospitali ya Rufaa ya KCMC inayomilikiwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) kukosa x-ray ya C.T scanner na kuwafanya wagonjwa kufuata vipimo hivyo kwenye hospitali nyingine.
Wameishangaa KCMC kukosa huduma muhimu na vifaa tiba vya kisasa vya uchunguzi wakati ni hospitali ya rufaa.
Hayo yaliibuliwa na Mwenyekiti Mtendaji wa shirika lisilo la kiserikali la taasisi ya kijamii ya utawala bora na maendeleo ( Cegodeta) Thomas Ngawaiya, wakati akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam jana.
Alisema Cegodeta imepokea malalamiko kutoka kwa wanachi walioidai kuwa wamekuwa wakihangaika kupata huduma za C.T. Scan na ultrasound katika hospitali hiyo.
Alisema ukosefu wa mashine hizo unasababisha usumbufu kwa wagonjwa ambao wakati mwingine hutumia kati ya Sh.200,000 hadi Sh.500.000 kutafuta vipimo hivyo.
Aliitaka serikali kuangalia upya sheria inayohusu hospitali za rufaa ili iwe na ulazima wa kuwapo vifaa tiba kwa wakati wote kwani kukosekana vipimo kwa wagonjwa itoshe kuiondolea sifa ya kuitwa hospitali ya rufaa.
"Mara nyingi wagonjwa wanapata usumbufu na wengine kupoteza maisha na wengine hushindwa kumudu gharama kubwa zinazokaribia Shilingi milioni, " alisema Ngawaiya.
Aliwaambia wanahabari kuwa Cegodeta imemwandikia barua Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk.Seif Rashid na kuambatanisha na vielelezo vyote vinavyoonyesha jinsi madaktari wanavyowaelekeza wagonjwa kwenda kufata vipimo kwenye sehemu nyingine na kurudi kwa matibabu.
"Hiyo inakuwa haina maana tena kama mgonjwa anatolewa katika hospitali ndogo na kupelekwa KCMC lakini cha ajabu anakosa huduma za vipimo na kuagizwa kufata huduma hizo sehemu nyingine, "alisema.
Waziri Rashid akizungumzia malalamiko hayo alisema KCMC haina vifaa hivyo na kueleza kuwa CT Scan ni mojawapo ya vifaa vinavyouzwa kwa bei kubwa lakini jitihada zinachukuliwa kusambaza huduma hizo ili kusaidia wananchi.
Aliutaka uongozi wa KCMC kununua vifaa vingine vinavyokosekana ikiwamo kipimo cha kuchunguza