Tukio hilo limetokea majira ya saa 5 asubuhi Leo na kudumu hadi Majira ya saa 10 jioni huku kituo cha Polisi kikivunjwa ,bunduki kuporwa na nyingine kuchomwa moto pamoja na magari matatu na Pikipiki Moja ya polisi.
Wakielezea tukio hilo wakazi wa mji wa Ilula wameueleza mtandao huu wa www.paparazihuru.com kuwa chanzo ni askari watatu akiwemo mkuu wa kituo cha Ilula kwenda kufanya msako wa wananchi wanaokunywa pombe muda wa kazi.
Hivyo kutokana na tukio hilo mwanamke huyo aliyepoteza Maisha aliyetambulika kwa jina la Mwanne Mtandi aliamua kukimbia kukwepa kukamatwa na Polisi hao Kabla ya kukutwa nyuma ya jengo la klabu hicho cha pombe za kienyeji kilichopo mtaa wa Ilala Mjini Ilula akiwa amekufa.
" Polisi hawa kila siku wamekuwa wakifika hapa klabuni na kukamata watu na siku kwanza walimkamata marehemu na kumtoza faini ya Tsh 20,000 na siku ya pili walimkamata yeye na mumewe na kuwatoza faini Tsh 40,000 na leo walikuwa wakija kumkamata tena na hapo ndipo mwanamke huyo aliamua kutimua mbio Kabla ya kukutwa amekufa" alisema shuhuda wa tukio hilo Shida Ngwata.
Huku Mkazi mwingine ambae hakutaka jina lake kutajwa hapa alisema kuwa Polisi hao walilazimika kutumia mabomu na risasi za moto kutokana na umati mkubwa wa watu waliojitokeza huku Moja Kati ya bomu likiokotwa ambalo lilikuwa halijalipuliwa.
Alisema kuwa askari watatu watatu ndio ambao walikuwa wakisakamwa na Raia hao ambao pia wamevunja vioo vya basi la Upendo kufuatia mkuu wa kituo Ilula kukimbilia ndani ya basi hilo wakati akifukuzwa na Raia hao .
Diwani wa kata ya Nyalumbu Ally kikunga alisema kuwa alipigiwa simu na wananchi wake kujulishwa juu na vurugu hizo na Baada ya kufika Eneo la tukio alikuta mwanamke huyo akiwa mahututi ila hakuweza kupata msaada toka kwa wananchi wengine ila kumkimbiza hospitali .
Diwani huyo alilishauri jeshi la Polisi kuacha kutumia nguvu zaidi Kwani alisema Eneo hilo la klabu ni Eneo ambalo pia wananchi wanapata mahitaji mbali mbali na kuwa mwanamke huyo alikuwa akifanya usafi katika chumba chake cha biashara ya pombe.
Hata hivyo alisema Raia hao wameharibu Mali mbali mbali pamoja na nyaraka zote na kuwafungulia mahabusu wote waliokuwemo mahabusu huku Lori Moja lililokamatwa kituoni hapo likilindwa kuharibiwa kuwa halina kosa.
Vurugu hizo zilisababisha wasafiri wanaotumia barabara ya Kuu ya Mikoa ya Nyanda za juu kusini kukwama kwa zaidi ya masaa 6 .
hili ni basi la Nyagawa linalofanya safari zake kutoka jijini dar - Njombe lilivyopasuliwa vioo na wananchi.
Japo mwandishi wa habari hizi alishuhudia magari mawili ya Polisi na Pikipiki yakiwa yamechomwa moto ,gari Moja la askari pia lilichomwa moto na magari mawili Moja la askari na daladala moja na basi la upendo kuharibiwa vibaya