Sunday, February 01, 2015

BREAKING NEWS: AJALI YAUA WATATU USIKU HUU ...NI BAADA YA KUGONGANA LORI NA BODA BODA NA kuteketea kwa moto-IRINGA



BREAKING NEWS: AJALI YAUA WATATU USIKU HUU ...NI BAADA YA KUGONGANA LORI NA BODA BODA NA kuteketea kwa moto-IRINGA
Hizi ndivyo  lori  hilo  lilivyoharibika

WATU   watatu   waliokuwa  wamepakizana mishikaki  wamekufa  kwa  kuteketea kwa moto  mjini  Iringa  usiku  huu  baada ya  usafiri aina ya  pikipiki (Boda  boda)waliyokuwa  wakisafiri  kutoka mjini Iringa  kuelekea Nduli nje  kidogo na  mji  wa Iringa  kugongana na lori aina ya  fusu  na  kupelekea  pikipiki  hiyo  kuwaka  moto.


Wananchi  wakishuhudia  ajali  hiyo  ya  Lori na boda  boda  leo usiku
Hii  ndio  pikipiki  iliyoteketea  kwa moto baada ya ajali
Ajali   hiyo  imetokea  majira ya saa  2 usiku  huu  wakati boda  boda hiyo  ikiwa katika mwendo mkali  kugongana na lori  hilo ambalo  pia  lilikuwa katika mwendo na  kusababisha   vifo  hivyo .
Mashuhuda  wa  tukio  hilo  waliozungumza na  mtandao  huu  wa  www.paparazihuru.com  wamesema  kuwa  kijana  mmoja  ambae  inasadikika  ndie  dereva  wa boda  boda  hiyo ametambuliwa kwa jina moja la  Julius huku  wengine  wawili  bado  kutambuliwa .
Kutokana na  ajali  hiyo mbali lori  hilo upande wa mbele  ngao yake  ilipinda   huku  eneo  hilo la mbele  likiharibika   vibaya  mfano wa  kugongana  gari kwa gari na  baada ya  hapo  pikipiki  hiyo  ilishika  moto  na kuteketea   yote  pamoja na watu hao  ambao  miili yao  ilizimwa kwa  mchanga  na  wasamaria wema.

Miili  ya  marehemu hayo  imehifadhiwa katika  chumba  cha maiti  cha  Hospitali  ya  Rufaa ya  mkoa  wa Iringa  kwa  utambuzi  zaidi