Tuesday, February 10, 2015

BARCELONA KUIVAA TANZANIA ALL STARS MACHI 28



BARCELONA KUIVAA TANZANIA ALL STARS MACHI 28
Timu ya wachezaji nyota wa zamani wa Barcelona,wanatarajia kuvaana na magwiji wa Tanzania,'Tanzania All Stars'kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Machi 28, mwaka huu.
Ujio huo mkubwa ni wa pili kutokea nchini ndani ya miezi sita iliyopita, ambapo Agosti mwaka jana magwiji wa Real Madrid walitua nchini na kucheza na magwiji wa hapa, mchezo ulioisha kwa Madrid kushinda mabao 3-0.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, mwakilishi wa wachezaji hao wa zamani wa Barcelona, Patrick Kluivert, alisema mechi hiyo itawahusisha wachezaji nyota wa Barcelona wakiwemo, Edgar Davids, Gaiza Mandieta, Ludovic Giuly, Francesco Coco na wengine wengi waliopitia klabu hiyo kwa miaka tofauti.