Tuesday, February 17, 2015

AJALI YAUA MWANAFUNZI DARASA LA KWANZA TUNDUMA MBEYA



AJALI YAUA MWANAFUNZI DARASA LA KWANZA TUNDUMA MBEYA
Baadhi ya wananchi pamoja askari polisi wakishangaa ajali hiyo katika eneo la Mwaka mji Mdogo wa Tunduma

Mmoja wa wananfunzi waliojeruhiwa katika ajali hiyo akiwa katika hospital ya serikali Tunduma


Mwanafunzi wa Darasa la kwanza katika shule msingi ya Umoja mjini Tunduma wilayani Momba aliyehamika kwa jina la Ibbu Sichwale  (6) amefariki dunia na Wengine Wawili wamejeruhiwa vibaya  katika ajari iliyo iliyohusisha gari aina ya lori lenye namba T120 BRA,T 705 CGG lililokuwa likitoka katika Maegesho ya magari ya  Lacy fagacy ilipo Mwaka Tunduma .

Tukio hilo limetokea katika eneo la Transforma lililo katika mtaa wa mwaka katika mji mdogo wa Tunduma Wilayani Momba Mkoani hapa.

Wote waliojeruhiwa katika ajili hiyo ni wanafunzi wa shule hiyo ambao majina yao hajafahamika mara moja ambapo hali zao bado ni mbaya nakwamba wamelazwa katika hospital ya serikali katika mji wa Tunduma momba mkoani mbeya  kwa matibu zaidi. 

 Wakizungumzia tukio hilo   Baadhi ya mashuhuda ambalo walikuwepo kwenye tukio hilo wamesema Watoto walikuwa wanavuka barabara kwenda ng`ambo ya pili huku wakiwa wameshikana mikono  ghafla gari lilitokezea likiwa na mwendo mkali baada kuona gari watoto hao waliachana ndipo mmoja alinusurika na mwingine alikufa papo hapo alisema mmoja wa mashuhuda hao.

Walisama baada ya dereva ambaye hakufahamika kwa jina mara moja  kusababisha mahafa hayo alisimamisha gari na kutoweka kwenda kusiko julikana kutokana na kuogopa kuuawa na wananachi wenye hasira kali.walisema hivyo.

Waliongeza kuwa  baada ya Dereva kukimbia Wakazi wengine walienda kukata mlija wa upepo  ambapo gari hilo lilianza kutembea lenyewe likielekea mtelemkoni  na kusababisha ajari  ya mtu mwingine wa tatu ambaye alisagwa miguu na inasadikika kuwa ana upungufu wa akili.

Mwili wa maremu umehifadhiwa katika Hospitari ya Serikali Tunduma na Wengine wamelazwa katika hospitari hiyo. pia Jeshi la polisi limethibitisha kutokea kwa ajari hiyo na linaendelea na uchunguzi ili kubaini chanzo cha ajari  hiyo nalinaendelea na  kumtafuta dreva wa gari hilo ili hatua stahiki zichukuliwe dhidi yake.