Wednesday, January 14, 2015

WATANZANIA WAASWA KUTOA USHIRIKIANO KATIKA SEKTA YA UWEKEZAJI



WATANZANIA WAASWA KUTOA USHIRIKIANO KATIKA SEKTA YA UWEKEZAJI
Mwenyekiti wa Wafanyabiashara wa Oman na Tanzania, Soud Ahmed Al-Rahili akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es salaam leo.

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii ,Dar

Watanzania wametakiwa kuonyesha ushirikiano katika sekta ya uwekezaji ili kuweza kuwavutia wawekezaji wa nje kuwekeza nchini.

Hayo yamesemwa leo na Mwenyekiti wa Wafanyabiashara wa Oman na Tanzania, Soud Ahmed Al-Rahili alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, wakati walipokuwa wakijadili masuala ya uwekezaji baina ya nchi ya Tanzania na Oman.

Al-Wahili amesema bidhaa za Tanzania zinazotarajiwa kupelekwa nchini Oman ni pamoja na nyama ya ng'ombe (Nyekundu) na Asali.Vitu hivyo vimekuwa na fursa katika soko la Oman hali ambayo watanzania waongeze juhudi ya kuzalisha kutokana na soko hilo kuwa pana na Tanzania ni nchi pekee inayoweza kunufaika na soko hilo.

Aidha  amesema  sekta ya uwekezaji ni pana kati ya Oman na Tanzania na ni wakati mwafaka kutumia fursa ya uwekezaji.