Thursday, January 15, 2015

watahiniwa 2,175 washindwa kufaulu mitihani ya Bodi ya Uhasibu na Ukaguzi (NBAA)



watahiniwa 2,175 washindwa kufaulu mitihani ya Bodi ya Uhasibu na Ukaguzi (NBAA)
Na Chalila Kibuda na Globu ya Jamii 

Imeelezwa kuwa watahiniwa 2,175 sawa na asilimia 46.9 wameshindwa kufaulu mitihani ya Bodi ya Uhasibu na Ukaguzi (NBAA).

Katika taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa NBAA,Pius Maneno ilisema kuwa mitihani hiyo ya kwanza katika mfumo mpya  wa elimu wa mafunzo unaozingatia weledi na matokeo hayo hayalinganishwi  na matokeo ya nyuma ilifanyika katika mfumo wa kukazia maarifa.

Kwa mujinu wa Maneno,watahiniwa waliojisajili ni 6,464  kati ya hao 678 sawa na asilimia 10.5 hawakuweza kufanya mtihani kwa sababu mbalimbali.

Taarifa hiyo imesema watahiniwa 1,260 wamefaulu mtihani ngazi husika ,watahiniwa 1,811  wamefaulu baadhi ya masomo  katika ngazi ngzi husika.

Jumla ya watahiniwa 356  ikiwa wanawake 95  na wanaume 261 wamefaulu mtihani wa shahada ya juu ya uhasibu nchini (CPA)  na kufikia watalaam  wa CPA 6002 tangu ianze mitihani hiyo mwaka 1975.