Tuesday, January 27, 2015

Tamko la UKAWA Laungwa mkono na Tume ya Warioba kususia kura ya maoni


Tamko la UKAWA Laungwa mkono na Tume ya Warioba kususia kura ya maoni
Wajumbe wa iliyokuwa Tume ya mabadiliko ya Katiba nchini Tanzania imeunga mkono tamko la umoja wa katiba ya wananchi UKAWA kwa kususia kushiriki katika mchakato wa upigaji wa kura ya maoni kuhusu kupitisha katiba mpya inayopendekezwa.


Wakizungumza katika mdahalo ambao umeitishwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere na kushirikisha baadhi ya wananchi wa mkoa wa Mara mjini Musoma, wajumbe hao wa iliyokuwa tume ya badiliko ya katiba wamesema pamoja na kutupwa kwa maoni ya wananchi, kukiukwa sheria katika mchakato wa katiba mpya pia muda uliobaki kwa ajili ya kutoa elimu kwa wananchi ili waweze kushiriki katika mchakato huo hautoshi hata kidogo.
  
Mjumbe mwingine aliyekuwa katika tume hiyo Bw Humphrey Polepole ameshangwazwa na baadhi viongozi waandamizi wa serikali wakiwemo marais wastaafu na mawaziri wakuu ambao amesema walitoa maoni kwa kupendekeza muundo wa serikali tatu wenye lengo la kuondoa malalamiko kati ya Tanganyika na Zanzibar ikiwa ni pamoja na kuimarisha muungano lakini wameshindwa kujitokeza hadharani kusema ukweli kuhusu jambo hilo.
  
Nao baadhi ya washiriki wa mdahalo huo, wameunga mkono tamko la UKAWA la kususia mchakato wa katiba huku wakimtaka Rais Jakaya Kikwete kusitisha kuendelea kwa mchakato huo, kwani wamesema kuendelea kwa mchakato wa kura ya maoni kamwe hakutawezesha kupatikana katiba bora na inayotakiwa na wananchi.