Wednesday, January 07, 2015

MBUNGE WA MOROGORO MJINI ATUMIA ZAIDI YA MILIONI 20 KUTATUA KERO YA MAJI KATA YA MLIMANI



MBUNGE WA MOROGOR MJINI ATUMIA ZAIDI YA MILIONI 20 KUTATUA KERO YA MAJI KATA YA MLIMANI
Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood Akisaini Kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili Kwenye Ofisi ya Mtendaji  kata ya Mlimani Katika Mfululizo wa Ziara zake katika Kata mbalimbali Jimbo la Morogoro mjini.

Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood Akikagua Vifuko vya mndihira na Mwere Vilivyo Kata ya mlimani Ambavyo Vimegarimu Kiasi cha Shilingi Milion 3 Zilizotolewa na Mbunge Huyo.
Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood Akianda Safu ya Milima Uluguru Kuelekea Mitaa ya Kisosa ,Choma na Chalagule vilivyopo Kata ya Mlimani 
 
Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood Akisikiliza kwa Makini Kero Mbalimbali zilizokuwa Zikiwasilishwa na wakazi wa Kata ya Mlimani Jimbo la Morogoro Mjini wakati Mbunge huyo aliopofanya ziara ya Kutembelea kata Hiyo.
Baadhi ya Wakazi wa Mitaa ya Ruvuma ,Mng'ong'o, na Tulo Iliyopo Kata ya Mlimani Wakimsikiliza kwa Makini Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini alipofanya ziara katika Mitaa hiyo ili kusikiliza kero mbalimbali zinazowakabili wakazi wa Kata hiyo.
Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood Akisisitiza Jambo wakati Akiongea na wakazi wa Kata ya Mlimani
Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood Akijibu Hoja Mbalimbali Mara baada ya  Kusikiliza Kero zinazowakabili wakati wa Kata  ya Mlimani  Ambapo walimwambia Wanakabiliwa na Kero Kubwa ya Umeme,Maji na Barabara.Kuhusu Maji Mh Abood alitoa Zaidi ya Shilingi Shilingi Milioni 20 Kwajili ya Kununua Vifaa vya Kuwezesha Kufikisha Maji katika Mitaa ya Kisosa ,Choma , Chalagule Ruvuma Mng'ong'o na Tulo Iliyopo Kata ya Mlimani. .Pia Alitoa vifaa vyenye Dhamani ya Shilingi Milion 2 kwajili  ya Kununua Vifaa vya Kukarabati Barabara  Za Mitaa hiyo Ikiwemo Sajuri,Makaravati na Vifaa vingine vinavyotumika kutengeneza Barabara.
  Wakazi waliojitokeza kwenye ziara ya Mbunge huyo
Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood Akipokea zawadi Kutoka kwa Wakazi wa Mitaa ya Kisosa ,Choma na Chalagule  Ikiwa ni Ishara ya kukubali Utendaji wa Kazi wa Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini.Wakielezea Zaidi wakazi hao wamesema Tangu Uhuru hakuna Mbunge aliyewahi kuwatembelea na pili Ahadi zote alizowahidi wakati wa Mitaa hiyo amezitekeleza na bado wana imani kubwa sana na Mbunge Huyo.Namnukuu Mkazi Mmoja aliyejitambuliza kwa Jina la Bw Omari Alisema " Huyu Ndiye Mbunge tunayemuhitaji Mbunge wa Vitendo na si Mbunge wa Maneno Mengi Utendaji Hafifu"
Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood Akiwa na mtendaji wa kata ya Mlimani mara baada ya kuwasili katika Mitaa ya Ruvuma Mng'ong'o na Tulo Iliyopo Kata ya Mlimani.
Wajumbe wa Serikali ya mtaa wakimsikiliza Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood 
Wakazi wa Mtaa wa Kikundi wakiwa Kwenye  Mvua Kumsikiliza Mbunge wao