Thursday, December 25, 2014

WANUSURIKA KUFA KUFUATIA AJALI YA GARI KIJIJI CHA MWIDU MKOANI MOROGORO


WANUSURIKA KUFA KUFUATIA AJALI YA GARI KIJIJI CHA MWIDU MKOANI MOROGORO
 
Camera ya GLOBU ya jamii ikiwa njiani kutoka Morogoro kuelekea jijini Dar,njia ilikutana ajali hii iliyotokea mapema jana kati ya gari ndogo aina ya NOAH ambayo namba zake za usajili hazikufahamika mara moja kufuatia kuharibika vibaya kutokana na ajali hiyo ya kugongwa kwa nyuma na basi la STAMILI kama lionekanavyo pichani lenye namba za usajili T43CJN lililokuwa likitokea Morogoro kuelekea jijini Arusha,Katika gari ya NOAH hakukuwemo na abiria zaidi ya dereva,ambaye alitoka mzima kama aonekavyo pichani (aliyeshika kiuno).

Ajali hiyo ilitokea katika kijiji cha Mwidu mkoani Morogoro,Mashuhuda wa ajali hiyo walieleza kuwa gari hiyo ndogo imetokana na basi la Stamili kuwa katika mwendo kasi na hatimae kuligonga gari hilo dogo kwa nyuma na kugonga Lori (halipo pichani).Katika ajali hiyo hakuna aliyepoteza maisha wala kujeruhiwa vibaya.

KAMANDA WA POLISI, KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI (T),MOHAMMED R.MPINGA – DCP amewataka kuwajulisha watumiaji wote wa barabara kuwa  askari wataendelea kuwa wakali sana katika kipindi hiki  ambapo hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa yeyote atakayekamatwa  akivunja sheria za usalama barabarani. ''Niwaombe tu watumiaji wote  wa barabara watii sheria bila shuruti'' alisema kamanda Mpinga huku akisisitiza kauli mbiu ya usalama barabarani kwa mwaka huu kuwa  

˝Maamuzi yako barabarani ni hatima yetu-Fikiria kwanza". . 
 Gari hiyo ndogo aina ya NOAH ikiondolewa barabarani
 Basi la STAMILI kama lionekanavyo pichani lenye namba za usajili T43CJN lililokuwa likitokea Morogoro kuelekea jijini Arusha
 Baadhi ya abiria waliokuwemo kwenye basi la STAMILI wakiwa kando kando ya barabara wakiwa hawaamini kilichotokea.
Polisi wa Usalama barabarani wakifanya kazi yao nzuri kabisa ya kuweka utaratibu wa kupunguza usumbufu kwa magari mengine wakati wa kupishana,huku magari yaliyokuwa kwenye ajali yakiondolewa na kupelekwa kituo cha polisi kwa mambo mengine ya kisheria za usalama barabarani