Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
Askofu Msaidizi wa Jimbo kuu la Katoliki ,Dar es Salaam Eusebius Nzigilwa amesema katika kuadhimisha sikukuu ya Krismas watu wafuate njia ya mungu na sio njia ya Ibilisi ambayo inafundisha maovu.
Akizungumza leo baada ya Ibada ya Sikukuu ya Krismas ,Nzigilwa alisema watu wenye uwezo lazima wasaidie wasio na uwezo kwani Yesu alizaliwa katika pango la Bethelehem lakini watu wenye uwezo walimuacha kutokana na kuwa katika njia ya ibilisi.
Nzigilwa alisema suala la kuingiziwa fedha katika akaunti yake ambazo zilitoka katika akaunti ya Tegeta Escrow hawezi kulizungumzia kwa sasa lakini siku zijazo atazungumzia suala hilo.
Naye Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT),Dk. Alex Malasusa alisema kuwa watu lazima wawe na hofu ya mungu mambo yanayotokea sasa ya ufisadi yanaiweka nchi sehemu mbaya.
Malasusa aliyasema hayo katika Ibada ya Krismas iliyofanyika katika Kanisa la Azania Front ,alisema nchi ipo katika mambo ambayo hayampendezi Mungu hivyo ni lazima tutoke huko ili wananchi waandokane na kusikia ufisadi kwani sio maendeleo ambayo yanatakiwa kwa sasa.
Mkuu wa Kanisa Kuu la St.Albano ,Aidano Mbulinyingi alisema jamii imeingia kufanya vitendo viovu kutokana na kuacha maandiko ya mungu hivyo tunahitaji kujenga msingi upya katika kutokomeza vitendo hivyo ambapo mungu hapendezi navyo.
Askofu Msaidizi wa Jimbo kuu la Katoliki ,Dar es Salaam Eusebius Nzigilwa akiongoza ibada ya Krismas katika Kanisa la Mt. Joseph,jijini Dar es salaam leo.
"Shkamoo....." Askofu Msaidizi wa Jimbo kuu la Katoliki ,Dar es Salaam Eusebius Nzigilwa akipokea salam kutoka kwa mtoto,mara baada ya Ibada ya Krismas katika Kanisa la Mt. Joseph,jijini Dar es salaam leo.
Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT),Dk. Alex Malasusa akiwatakia heri ya Krismas sehemu ya Waumini wa Kanisa la KKKT Azania Front,jijini Dar es Salaam leo.