Wahitimu wa digrii ya elimu jamii katika taaluma za maendeleo jamii wakishangilia baada ya Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU), Cleopa Msuya kuwatunuku katika mahafali ya 8 ya chuo hicho, kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam jana.
Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU), Cleopa Msuya akimtunuku Digrii ya Uzamifu, Rigobert Buberwa, wakati wa mahafali ya 8 ya Chuo hicho, Dar es Salaam. Buberwa ametunukiwa digrii hiyo baada ya kufanikiwa kufanya utafiti unaohusu "Kuelekea modeli ya mfumo wa kompyuta wa kutunza taarifa za ardhi na mabadiliko ya umiliki wake: Nyenzo mpya ya Usimamizi wa Ardhi nchini Tanzania." PICHA ZOTE NA KAMANDA MWAIKENDA WA KAMANDA WA MATUKIO BLOG
Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU), Cleopa Msuya akimtunuku Digrii ya Uzamifu (Doctor of Phylosophy Degree), Deusdedit Kibassa, wakati wa mahafali ya 8 ya Chuo hicho, yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam leo.Mada ya utafiti aliyoifanya inahusu: "Umuhimu wa kutumia maeneo ya kijani kupunguza athari zitokanazo na kuongezeka kwa hali ya joto katika maeneo ya katikati ya Jiji la Dar es Salaam."
Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU), Cleopa Msuya akimtunuku Digrii ya Uzamifu, Dawah Mushi, wakati wa mahafali ya 8 ya Chuo hicho, yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam. Mada ya utafiti aliyoifanya Mushi inahusu: "Uhamishwaji wa makazi ya watu wengi waliobomolewa makazi yao katika mradi wa upanuzi wa Uwanja wa Ndege jijini Dar es Salaam."
Daniel Mbisso akitunukiwa Digrii ya Uzamifu
Joel Msami akitunukiwa Digrii ya Uzamifu
Eliwaha Msangi akitunukiwa Digrii ya Uzamifu
Margareth Ntiyakunze akitunukiwa Digrii ya Uzamifu
Sara Phoya akitunukiwa digriii ya uzamifu
Baadhi ya wahitimu wakipiga picha wakati wa mahafali hayo
Bendi ya JKT ikiongoza maandamano ya viongozi na wahadhili wa chuo hicho kuingia ukumbini
Wahadhiri na viongozi wakiingia kwa maandamano kwenye ukumbi
baadhi ya wahitimu wakisubiri kutunukiwa digrii
Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu Ardhi, Tabitha Siwale akihutubia katika mahafali hayo
Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Idrissa Mshoro akihutubia wakati wa mahafali hayo
Wahitimu wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU), wakiweka kofia kichwani ikiwa ni ishara ya kutunukiwa digrii ya uzamili ya sayansi ya usimamizi na uchumi ujenzi, wakati wa mahafali ya 8 ya Chuo hicho, yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam
Ni furaha iliyoje baada ya kutunukiwa
Baadhi ya ndugu jamaa na marafiki wa wahitimu wakiwa katika mahafali hayo
Waziri Mkuu wa zamani, ambaye ni Mkuu wa Chuo cha ARU, Cleopa Msuya akitoka baada ya mahafali hayo kumalizika leo
Msuya akiongoza maandamano kutoka nje baada ya mahafali hayo kumalizika
Hali ilivyokuwa nje ya ukumbi wa Diamond Jubilee baada ya mahafali kumalizika