Thursday, December 18, 2014

Wafanyakazi Vodacom watembelea wagonjwa CCBRT



Wafanyakazi Vodacom watembelea wagonjwa CCBRT
Mtoto Raphael Barnaba (4) kutoka mkoani Mbeya anayetibiwa miguu katika hospitali ya CCBRT iliyopo jijini Dar es Salaam, akipokea kwa furaha zawadi ya matunda kutoka kwa mfanyakazi wa kampuni ya simu ya Vodacom kitengo cha Rasilimali Watu, Alice Lewis (katikati) wakati wafanyakazi wa kampuni hiyo walipotembelea wagonjwa katika hospitali hiyo na kuwagawia matunda kama sehemu ya kampeni ya Pamoja na Vodacom chini ya Vodacom Foundation wakati wa kipindi hiki cha sikukuu za mwisho wa mwaka. Akitazama ni mama wa mtoto huyo (wa kwanza kushoto).
Meneja biashara wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Grace Lyon(kushoto)akimuongelesha jambo Mtoto Elisha Lazaro(5) kutoka mkoani Mbeya anayetibiwa miguu katika hospitali ya CCBRT iliyopo jijini Dar es Salaam, wakati wafanyakazi wa kampuni hiyo walipotembelea wagonjwa katika hospitali hiyo na kuwagawia matunda kama sehemu ya kampeni ya Pamoja na Vodacom chini ya Vodacom Foundation wakati wa kipindi hiki cha sikukuu za mwisho wa mwaka.
Mfanyakazi wa Vodacom Tanzania Neema Kisanga akiwapatia zawadi za matunda wakina mama wanaotibiwa Fistula katika hospitali ya CCBRT iliyopo jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya kampeni ya Pamoja na Vodacom chini ya Vodacom Foundation wakati wa kipindi hiki cha sikukuu za mwisho wa mwaka.
Mmoja wa kinamama Lucy John anaetibiwa Fistula katika hospitali ya CCBRT iliyopo jijini Dar es Salaam, akipokea zawadi ya matunda kutoka kwa mfanyakazi wa kampuni ya simu ya Vodacom kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Umma, Glory Mtui(kulia)wakati wafanyakazi wa kampuni hiyo walipotembelea wagonjwa katika hospitali hiyo na kuwagawia matunda kama sehemu ya kampeni ya Pamoja na Vodacom chini ya Vodacom Foundation wakati wa kipindi hiki cha sikukuu za mwisho wa mwaka.
Meneja wa Ruzuku na Mawasiliano wa Vodacom Foundation Renatus Rwehikiza(kushoto)akimkabidhi zawadi ya matunda Joyce Mwenda anaetibiwa Fistula katika hospitali ya CCBRT iliyopo jijini Dar es Salaam,wakati wafanyakazi wa kampuni hiyo walipotembelea wagonjwa katika hospitali hiyo na kuwagawia matunda kama sehemu ya kampeni ya Pamoja na Vodacom chini ya Vodacom Foundation wakati wa kipindi hiki cha sikukuu za mwisho wa mwaka na katikati ni Aisha Shabani.
Mfanyakazi wa Vodacom Tanzania Protas Ruwanda(kushoto) akimkabidhi zawadi ya matunda Hawa Othmani anaetibiwa Fistula katika hospitali ya CCBRT iliyopo jijini Dar es Salaam,wakati wafanyakazi wa kampuni hiyo walipotembelea wagonjwa katika hospitali hiyo na kuwagawia matunda kama sehemu ya kampeni ya Pamoja na Vodacom chini ya Vodacom Foundation wakati wa kipindi hiki cha sikukuu za mwisho wa mwaka na katikati ni Joyce Mwenda.
Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakiwasili katika hospitali ya CCBRT walipotembelea wagonjwa katika hospitali hiyo na kuwagawia matunda kama sehemu ya kampeni ya Pamoja na Vodacom chini ya Vodacom Foundation wakati wa kipindi hiki cha sikukuu za mwisho wa mwaka.

Wakina mama na wanaotibiwa katika Hospitali ya CCBRT iliyopo Msasani jijini Dar es Salaam,wametembelewa na baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom na kupatiwa msaada wa vyakula mbogamboga na matunda kwa wagonjwa wenye mahitaji ambao wanatibiwa katika hospitali ya CCBRT iliyopo jijini Dar es Salaam.

Msaada huo umekabidhiwa leo kwa uongozi wa hospitali hiyo ambapo pia wafanyakazi wa kampuni hiyo walipata fursa ya kuwatembelea wagonjwa  waliolazwa na kuwafariji ikiwemo kuwagawia matunda,na zawadi mbalimbali.

Meneja wa Ruzuku na Mawasiliano wa Vodacom Foundation Renatus Rwehikiza amesema kampuni ya Vodacom kupitia taasisi yake ya Vodacom Foundation mwaka huu katika kuelekea katika sikukuu ya Krismas na mwaka mpya imeona ni muhimu kuwakumbuka wagonjwa ambao wamelazwa hospitalini ili kuwasaidia nao wapate faraja na kujisikia kama sehemu ya jamii.

"Tunajua kuwa kuna makundi mengi ya wahitaji katika jamii hivyo tumeona safari hii tuangalie kundi la wagonjwa waliolazwa hospitalini ambao wana mahitaji makubwa ili waweze kupona maradhi yanayowasumbua waweze kuendelea na maisha yao ya kawaida  na siku kusaidia makundi ya  wahitaji kwenye jamii ''.Alisema Bi Verma.

Alisema safari hii badala ya kutoa vifaa kwa hospitali wamelengwa wagonjwa ambapo wamepatiwa vyakula,matunda va vyakula vya lishe ili kuwawezesha kupata lishe bora inayohitajika katika miili yao katika kipindi hiki kigumi kwao wanapoendelea kupata matibabu ili kurejesha afya zao kama zilivyokuwa hapo awali.

Muuguzi na Mshauri katika wodi ya akina mama wanaotibiwa Fistula hospitalini hapo,Bi Theodora Millinga,  aliishukuru Vodacom kwa kuwakumbuka wagonjwa na alisema kuwa  ana imani walengwa wa msaada huu wamepata faraja kubwa kwa kupatiwa msaada huu wa lishe ambao ni wa muhimu katika kipindi cha matibabu. 

"Tunashukuru kwa kufika kuwafariji wagonjwa hawa na natoa wito kwa akina mama wenye ugonjwa huu wa Fistula wajitokeze kupata matibabu pia jamii ielewe kuwa huu ni ugonjwa kama yalivyo magonjwa mengine na iache kuwanyanyapaa waathirika".Alisisitiza.

Baadhi ya wagonjwa waliolazwa CCRBT walishukuru kampuni ya Vodacom na wafanyakazi wake kwa kufika kuwafariji na kuwapatia msaada wa vyakula vya lishe.

Vodacom kupitia taasisi yake ya Vodacom Foundation imekuwa ikitoa  misaada mbalimbali ya kuleta mabadiliko kwenye jamii hususan katika sekta ya elimu na Afya bila kusahau makundi yenye mahitaji maalumu kwenye jamii

Baadhi ya wagonjwa waliolazwa CCBRT walishukuru kampuni ya Vodacom naa wafanyakazi wake kwa kufika kuwafariji na kuwapatia msaada wa vyakula vya lishe.


Vodacom kupitia taasisi yake ya Vodacom Foundation imekuwa ikitoa  misaada mbalimbali ya kuleta mabadiliko kwenye jamii hususan katika sekta ya elimu na Afya bila kusahau makundi yenye mahitaji maalumu kwenye jamii