Thursday, December 18, 2014

UTT-AMIS YATOA ELIMU YA MIFUKO YA UWEKEZAJI WA PAMOJA KWA MADAKTARI



UTT-AMIS YATOA ELIMU YA MIFUKO YA UWEKEZAJI WA PAMOJA KWA MADAKTARI


Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano wa UTT-AMIS, Daudi Mbaga akitoa mada kuhusu Mifuko ya Uwekezaji wa Pamoja UTT-AMIS  katika mkutano Mkuu wa 47 wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT) uliofanyika katika Ukumbi wa Pius Msekwa mjini  Dodoma hivi karibuni. Mkutano huo ulidhaminiwa na UTT-AMIS
Washiriki wa semina hiyo.
urugenzi wa Masoko na Uhusiano wa UTT AMIS, Daud Mbaga akitoa mada katika mkutano Mkuu wa 47 wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT)
 Baadhi ya washiriki wa semina ya Wanachama wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT) wakifuatilia mada iliyokuwa ikitolewa kuhusu Mfuko wa Dhama ya Uwekezaji wakati wa semina ya Wanachama Chama cha Madaktari.

Na Mwandishi Wetu
MADAKTARI wametakiwa kujitokeza katika masuala ya uwekezaji kwani fursa hiyo wanayo kama ilivyo kwa baadhi ya watu kutoka nje.
 
Hayo yalisemwa na Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano wa UTT- AMIS, Daudi Mbaga wakati akitoa mada katika Mkutano wa 47 wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT) uliofanyika katika Ukumbi wa Pius Msekwa mjini Dodoma na kudhaminiwa na Mfuko wa Dhamana ya Uwekezaji UTT-AMIS.

Alisema kutokana na baadhi ya watu hapa nchini kudhani kuwa ili mtu awe muwekezaji ni lazima atoke nje ya nchi wakati sio kweli.
"Nawaomba madaktari mtambue kuwa ni sehemu ya wawekezaji hivyo basi msijitenge mnaposikia fursa kama hizi na badala yake mjitokeze katika mfuko huu wa UTT," alisema Mbaga.
Alisema kuwa wameamua kufikisha elimu kuhusu mfuko wa Dhamana ya Uwekezaji kwa madaktari kwani anaamini itawajengea uwezo wa uwelewa kuhusu jinsi ya kuwekeza.
Mbaga aliongeza kuwa Mfuko wa Umoja ulianzishwa mwaka 2005, ni mfuko unaolenga kutimiza mahitaji tofauti ya wawekezaji huku ukitoa faida.Alizitaja baadhi ya faida hizo kuwa ni uwekezaji ulio wazi kwa kila mtanzania; vipande vinauzwa kwa bei ya soko (hakuna ada ya kujiunga).Nyingine ni mwekezaji anaweza kununua vipande kumi, kuna urahisi wa kujiunga na kujitoa wakati wowote pindi mwekezaji anapotaka kufanya hivyo.