Thursday, December 18, 2014

TAASISI YA WANAWAKE NA MAENDELEO (WAMA) YAANDAA MKUTANO WA WATAALAM NA WADAU WA USONJI (AUTISM)

TAASISI YA WANAWAKE NA MAENDELEO (WAMA) YAANDAA MKUTANO WA WATAALAM NA WADAU WA USONJI (AUTISM)
 Mkurugenzi wa Idara ya Uboreshaji Afya kutoka Taasisi ya Wamnawake na Maendeleo, WAMA, Dkt. Sarrah Maongezi akiwasilisha mada kwenye mkutano maalum wa wadau mbalimbali wa usonji (Autism) uliofanyika jijini Dar es Salaam tarehe 16.12.2014 ili kuzungumzia hali halisi ya tatizo la usonji na changamoto zake hapa nchini ili kujenga mfumo bora wa huduma kwa watoto wenye usonji.

 Daktari Kissah Mwambene kutoka Chama cha Madaktari wa Afya ya Akili (MEHATA) akitoa uzoefu wa chama chao katika kushughulikia masuala ya watoto walio na usonji hapa nchini kwenye mkutano wa wataalam na wadau wa ugonjwa huo uliofanyika\ tarehe 16.12.2014.

 Makamu wa Rais Mwandamizi Profesa Andy Shih anayeshughulikia masuala ya sayansi kutoka Shirika la Kimataifa linaloshughulikia uboreshaji wa huduma kwa watu wenye matatizo ya usonji duniani,( Autism Speaks) akitoa taarifa kuhusu shughuli na miradi ya  Shirika hilo lenye makao makuu yake New York nchini Marekani.

 Katibu wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Ndugu Daud Nassib akiongoza majadiliano kwenye mkutano wa wataalam na wadau wa Usonji uliofanyika jijini Dar es Salaa tarehe 16.12.2014.

 Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, Mama Salma Kikwete akimkaribisha kwa mazungumzo Profesa Andy Shih, Makamu wa Rais Mwandamizi kutoka Shirika la Autism Speaks aliyemtembelea Mama Salma ofisini kwake
 Mke wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA, Mama Salma Kikwete akizungumza na wajumbe wa mkutano maalum ulioandaliwa na Taasisi yake kuhusu tatizo la hapa nchini.
 Mke wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA, Mama Salma Kikwete akizungumza na wajumbe wa mkutano maalum ulioandaliwa na Taasisi yake kuhusu tatizo la hapa nchini.
 Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Makamu wa Rais Mwandamizi Profesa Andy Shih anayeshughulikia masuala ya sayansi kutoka shirika la Autism Speaks lenye Makao Makuu yake huko New York nchini Marekani. Profesa Shih akifuatana na Dkt. Kra Reagan walimtembelea Rais Kikwete huko Ikulu 
 ais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Makamu wa Rais Mwandamizi Profesa Andy Shih anayeshughulikia masuala ya sayansi kutoka shirika la Autism Speaks lenye Makao Makuu yake huko New York nchini Marekani. Profesa Shih akifuatana na Dkt. Kra Reagan walimtembelea Rais Kikwete huko Ikulu 
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akifanya mazungumzo na Profesa Andy Shih aliyemtembelea huko Ikulu  
PICHA NA JOHN LUKUWI.