Friday, December 05, 2014

TAARIFA YA KUKOSEKANA HUDUMA YA MAJI KWA WAKAZI WA MLANDIZI, KIMARA NA TABATA


TAARIFA YA KUKOSEKANA HUDUMA YA MAJI KWA WAKAZI WA MLANDIZI, KIMARA NA TABATA
Shirika la Maji Safi na Majitaka Dar-es-salaam (DAWASCO), linawatangazia  wakazi wa KIMARA na TABATA; Miji ya Kibaha na Mlandizi mkoani Pwani  kuwa, Mtambo wa kuzalisha Maji wa Ruvu Juu umepata hitilafu kuanza siku ya Jumatano ya tarehe 03.12.2014 baada ya kuharibika kwa pampu moja ya kusukuma Maji (Pre-lift pump). 

Hali hii imelazimisha kupungua kwa uzalishaji Maji. 

Mafundi wa DAWASCO wanaendelea na matengenezo na kuhakikisha Pampu hii inafanya kazi na Huduma ya  Maji itarejea katika hali ya kawaida ifikapo siku ya Jumapili tarehe 07/12/2014
Wakazi wa maeneo yafuatayo wataathirika; MLANDIZI, KIBAHA, KIBAMBA, MBEZI, KIMARA, UBUNGO, MSEWE, KIBANGU, RIVERSIDE, BARABARA YA MANDELA, TABATA, NA SEGEREA.

PIGA SIMU KITUO CHA HUDUMA KWA WATEJA NAMBA 022- 2194800/ 0659-574012
DAWASCO INAWAOMBA RADHI KWA USUMBUFU AMBAO NI WA DHARULA.

IMETOLEWA NA OFISI YA UHUSIANO
DAWASCO-MAKAO MAKUU
"DAWASCO TUTAKUFIKIA"