Friday, December 05, 2014

MAMA ALIYETELEKEZWA NA MUMEWE AOMBA MSAADA KWA WASAMALIA WEMA


MAMA ALIYETELEKEZWA NA MUMEWE AOMBA MSAADA KWA WASAMALIA WEMA
WANAWAKE wengi duniani bado wananyanyaswa kijinsia kwa sababu za kijamii, kiuchumi na kipato licha ya kuwepo kwa elimu kuhusu haki zao.


Mwanamama Ester Charles ambaye ni mkazi wa Mwambani wilayani Ilemela ametelekezwa na mumewe aliyetajwa kwa jina la Albinus na kubakizwa na watoto wawili wadogo wanaohitaji uangalizi na usimamizi. Pichani mwanamama Ester akiwa na mtoto wake mdogo anayetaabika na ugonjwa wa kupooza. 



KWA UFUPI

Mumewake alipopata mwanamke mwingine alihama nyumba aliyokuwa akiishi na mama huyu na kupanga eneo jingine kabisa bila kuikumbuka familia yake katika matumizi na mahitaji muhimu.
Alipomfikisha mumewe huyo mbele ya mikono ya Sheria alikubali kutoa huduma lakini ndani ya kipindi kifupi alitorokea kusikojulikana.
Amefika kuomba msaada toka kwa wasamalia wema watakaoguswa na simulizi yake. BOFYA PLAY KUSIKILIZA. 
Hali ya afya ya kwa mtoto Jr. Albinus si ya kuridhisha na haijafahamika nini kinachomsibu kwani bado hajafika hospitali kupata matibabu ya kina. Mtoto huyu pichani hawezi kutembea, hawezi kuzungumza kwa ufasaha wala kukaa, zaidi ya kulala tu muda wote.


CHANGAMOTO ALIZONAZO MAMA ESTER.

Hana pesa kwaajili ya chakula cha watoto.
Hana nguo kwaajili ya kuwavisha watoto na yeye binafsi.
Anadaiwa pesa ya kulipia nyumba anayoishi kiasi kwamba mwenye nyumba anataka kumfukuza.
Amejaribu kuomba kazi kwenye kaya mbalimbali na kukosa, akipewa majibu kuwa hawezi kuajiriwa akiwa na watoto (atashindwa kufanya majukumu ya mwajiri) naye hana sehemu ya kuwahifadhi iwe ndugu au majirani.
Jeh! Umeguswa tafadhali wasiliananaye kupitia namba 0753804881.

MUNGU AWABARIKI.