Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Profesa Salome B. Misana (pichani) kuwa Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira ( NEMC). Profesa Misana ni Mhadhiri Mwandamizi toka Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam. Uteuzi huo umeanza rasmi tarehe 4/12/2014.
Wakati huo huo , Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Mazingira, Dkt. Binilith Mahenge amewateua Wajumbe wa Bodi hiyo .
Walioteuliwa ni Profesa Reuben Mwamakimbulah kutoka Chuo kikuu cha Sokoine Morogoro, kitivo cha Misitu na Utunzaji wa mazingira, Injinia Bengiel Humphrey Msofe ambaye ni Mkurugenzi wa huduma za ufundi kutoka Wizara ya Nishati na Madini , Bi Judica Haikase Kida Omari, Kamishna Msaidizi kutoka Wizara ya fedha na Uchumi.
Wajumbe wengine walioteuliwa ni Injinia Frida Rweyemamu, Mkuu wa Idara ya maji vijijini kutoka Wizara ya Maji, Ndugu Sheha Mjaja Juma Mkurugenzi Idara ya Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Juma Mgoo ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii , Bi Anna William Mtani, Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Miji kutoka Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).
Mwingine ni Julius Keneth Ningu kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais yeye ni Mkurugenzi Idara ya Mazingira . Uteuzi huo unaanza rasmi tarehe 18/12/2014
Imetolewa na
KATIBU MKUU
OFISI YA MAKAMU WA RAIS