Friday, December 05, 2014

Msama Video Productions yajipanga Tamasha la Krismasi



Msama Video Productions yajipanga Tamasha la Krismasi
index
KAMPUNI ya Msama Video Productions imetoa tamko kwamba mwaka huu wamejipanga vizuri kufikisha ujumbe wa neon la Mungu katika Tamasha la Krismas kwani wanavifaa vipya na vya kisasa vyenye uwezo mkubwa wa kufanya kazi katika mazingira yoyote yale na wafanyakazi wakutosha wenye weledi katika fani hiyo.

Akizungumza jijini Dar 
, Meneja wa kitengo hicho, Alpha Kigalla alieleza sababu za kufanikisha vilivyo katika tamasha hilo ni kwa sababu ya umahiri wa  watendaji wa kirengo hicho ndio chachu itakayofanikisha kutekeleza ibada hiyo kwa waumini na mashabiki watakaojitokeza katika Tamasha hilo.

Kigalla alitoa wito kwa wakazi wa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini kujitokeza kwa wingi kushuhudia kazi za kitengo hicho kilicho katika kampuni ya Msama kwani wana vifaa vya kisasa zaidi.

"Msama Video Productions ina vifaa vipya na vya kisasa zaidi  na hata watendaji wake wako makini zaidi na utekelezaji wa kazi zao, hivyo wadau wa muziki nchini kujitokeza kufanikisha kazi zao," alisema Kigalla.


Meneja huyo alisema wakazi wa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini kujiandaa na kazi bora za Msama Video Productions ambazo zitafanikishwa kupitia waimbaji mbalimbali wa muziki huo.