KIKOSI cha Usalama Barabarani nchini kwa kushirikiana na Chama cha Kutetea Abiria Tanzania (CHAKUA) limesema wataendelea kudhibiti upandishaji wa holela wa nauli za mikoani kuelekea katika sikukuu za kufunga mwaka.
Akizungumza na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa idara ya habari Maelezo Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani,Mohamed Mpinga amesema watachukua hatua kali kwa mawakala wataopandisha nauli za mikoani.
Mpinga alisema kikosi cha usalama barabarani kimejipanga kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora usafiri kwa bei zilizopangwa pamoja na kutoa onyo kwa madereva wanaoendesha mabasi na magari kufuata sheria za usalama barabarani.
"Hatutavumilia mawakala na madereva watakaokiuka sheria za usalama barabarani yote haya ni kutaka wananchi wetu wasinyanyasike katika kipindi cha sikukuu siku zijazo sheria zimewekwa na lazima watu wazifuate"alisema ,Mpinga.
Aidha alisema wananchi wanatakiwa kutoa ushirikiano pale watapoona wanaopandisha nauli ili kuweza sheria ichukue mkondo wake kukaa kimya kwa wananchi kunafanya jeshi kushindwa kuwabana watu wanaofanya hivyo.
Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Mohamed R. Mpinga akizungumza na waandishi wa habari kuhusu abiria kutoa taarifa kwenye mamlaka husika ili watetewa na fedha zao ziweze kurudishwa hata kama ni Tsh. 100/=.