Monday, December 22, 2014

Mhe .Ummy Mwalimu Aendesha Mafunzo ya Kuwajengea Uwezo Wasichana wa Wilaya ya Muheza - Tanga


Mhe .Ummy Mwalimu Aendesha Mafunzo ya Kuwajengea Uwezo Wasichana wa Wilaya ya Muheza - Tanga
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tanga na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais,Mhe Ummy Mwalimu kupitia Taasisi ya Maendeleo ya Wanawake wa Mkoa wa Tanga (TAWODE) ameendesha mafunzo ya kuwajengea uwezo wasichana wa Wilaya ya Muheza, Mkoani Tanga wenye umri kati ya miaka 10 - 24. Lengo la mafunzo hayo ni kuwawezesha wasichana hao kujitambua na kujithamini katika masuala ya afya ya uzazi ili kujikinga na mimba na ndoa za utotoni na maambukizi ya VVU/UKIMWI.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tanga na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais,Mhe Ummy Mwalimu akifungua mafunzo kwa wasichana wa Wilaya ya Muheza juu ya kujitambua na kujithamini katika masuala ya Afya ya uzazi. Mafunzo hayo yamefanyika mwishoni mwa wiki Wilayani Muheza.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tanga na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais,Mhe Ummy Mwalimu akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo ya kujitambua na kujithamini Wilayani Muheza mwishoni mwa wiki.
Wasichana wa Wilaya ya Muheza wakifanya majadiliano na mawasilisho katika vikundi juu ya changamoto wanazokumbana nazo katika kipindi cha ujana.