Thursday, December 18, 2014

MHE. DKT PINDI CHANA AZINDUA SEMINA YA KUDUMISHA AMANI NA KUKOMESHA VITENDO VYA UKATILI ROLYA, MARA



MHE. DKT PINDI CHANA AZINDUA SEMINA YA KUDUMISHA AMANI NA KUKOMESHA VITENDO VYA UKATILI ROLYA, MARA
Mheshimiwa Dkt.Pindi Chana (Mb.) Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto tarehe 17/12/2014 alifungua rasmi semina maalum kuhusu masuala ya kukomesha vitendo vya Ukatili na kudumisha Amani Mkoani Mara.

 Semina hiyo ilindaliwa na kanisa la Anglikana Tanzania Dayosisi ya Rorya , Kanisa kuu Mt. Petro Kowak, kata ya Nyathorogo.

Wakati wa ufunguzi wa Semina hiyo Mheshimiwa Naibu Waziri aliwasihi wadau mbalimbali wa maendeleo ya Jinsia kutekeleza kwa vitendo kauli Mbiu Siku ya Mtoto wa Kike Duniani, inayosema "Maisha Yangu,Haki Yangu, Piga Vita Ndoa za Utotoni"

Alieleza kuwa Suala la ndoa za utotoni na ukeketaji linatia dosari kubwa katika harakati za kumkomboa mtoto wa kike kwa vile taifa linahitaji mchango wa kila mwananchi ili kufikia malengo yake ya kujiletea maendeleo sambamba na utekelezaji wa Malengo ya Mpango wa Taifa wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini( MKUKUTA), Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025 na Malengo ya Milenia, hivyo ndoa za utotoni na ukeketaji zinapaswa  kupigwa vita kwa nguvu zote na jamii yote.

Aidha, akiwa Mkoani Mara, Mheshimiwa Dkt.Pindi Chana (Mb.) alitembelea Chuo cha Maendeleo ya Jamii Buhare, Musoma.
Mhe. Dkt Pindi Chana (Mb.) akitoa hotuba ya Ufunguzi wa Semina kuhusu Masuala ya Ukeketaji na kudumisha Amani, Rolya Mara.
Mhe. Dkt Pindi Chana (Mb.) akiwa na Askofu wa Kanisa la Anglikana Tanzania, Dayosisi ya Rolya, wakati wa Ufunguzi wa Semina kuhusu Masuala ya Ukeketaji na kudumisha Amani, Rolya Mara.
Mhe. Dkt Pindi Chana (Mb.) akiwa na viongozi wa Serikali ya Mkoa wa Mara na Wilaya ya Rolya, wakati wa Ufunguzi wa Semina kuhusu Masuala ya Ukeketaji na kudumisha Amani, Rolya Mara.
Mhe. Dkt Pindi Chana akiwa katika picha ya Pamoja na Watumishi wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Buhare, Musoma.