Makamu wa Rais wa                Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib                Bilal, akizungumza wakati wa hafla fupi iliyofanyika leo                Desemba 26, 2014 kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es                Salaam ya kuwaaga jumla ya watoto 55 wenye matatizo ya                ugonjwa wa Moyo kati ya 104, waliofadhiliwa na Lions Club                ya jijini, kwa ajili ya kwenda kutibiwa nchini India.                Watoto hao 55 wa awamu ya kwanza wanaanza kuondoka nchini                leo. 
                Makamu wa Rais wa                Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib                Bilal, akiteta jambo na Rais wa Lions (Host) Club ya Dar                es Salaam, Mathew Levi, wakati wa hafla fupi ya kuwaaga                watoto 55 wenye matatizo ya ugonjwa wa Moyo kati ya 104,                kwa ajili ya kwenda kutibiwa nchini India. Watoto hao 55                wa awamu ya kwanza wanaanza kuondoka nchini leo.
                Makamu wa Rais wa                Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib                Bilal, akisalimiana na mmoja kati ya watoto wanaokwenda                kutibiwa nchini India, wakati wa hafla fupi ya kuwaaga                watoto hao wenye matatizo ya ugonjwa ya moyo iliyofanyika                leo Desemba 26, 2014 kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es                Salaam.
                Makamu wa Rais wa                Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib                Bilal, akivishwa Beji ya miaka 50 ya Lions Club na Makamu                wa Gavana wa Club hiyo, kwa nchi za Tanzania na Uganda,                Hyderali Gangji, wakati wa hafla fupi ya kuwaaga watoto                wenye matatizo ya ugonjwa wa moyo wanaokwenda nchini India                kutibiwa. Hafla hiyo ilifanyika leo Desemba 26, 2014                kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. 
                Makamu wa Rais wa                Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib                Bilal, akimkabidhi zawadi mtoto, Nabil Hahya (4) kutoka                Jijini Dar es Salaam, mmoja kati ya watoto 55 wa awamu ya                kwanza kati ya 104 wenye matatizo ya ugonjwa wa Moyo                wanaokwenda kutibiwa nchini India, wakati wa hafla fupi ya                kuwaaga watoto hao iliyofanyika leo Desemba 26, 2014                kwenye Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni                Mama wa motto huyo, Amina Yahya. 
                Makamu wa Rais wa                Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib                Bilal, akiagana na baadhi ya wadau wa Lions Club, baada ya                hafla fupi ya kuwaaga watoto hao. 
                Makamu wa Rais wa                Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib                Bilal, akimkabidhi zawadi mtoto, Hyria Ally (miezi 9)                Kutoka Zanzibar, mmoja kati ya watoto 55 wa awamu ya                kwanza kati ya 104 wenye matatizo ya ugonjwa wa Moyo                wanaokwenda kutibiwa nchini India, wakati wa hafla fupi ya                kuwaaga watoto hao iliyofanyika leo Desemba 26, 2014                kwenye Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni                Mama wa motto huyo, Zulekha Said. 
                                        Badhi ya watoto hao                wenye matatizo ya ugonjwa wa moyo, wakiwa na mama zao                wakati wa hafla hiyo.
                Baadhi ya wadau                waliohudhuria hafla hiyo. Picha na OMR 
        











