Mpendwa baba Alex Safi Maridadi, ingawa umetutoka kimwili miaka 26 iliyopita, tunasheherekea zawadi ya maisha Mungu aliyokujalia na uwepo wako katika maisha yetu. Tunakumbuka upendo, ukarimu na uongozi wako katika familia. Unakumbukwa na mke wako mpendwa Therese Maridadi, watoto wako, wajukuu, ndugu, jamaa na marafiki wote.
Bwana akupatie pumziko la milele, na mwanga wa milele akuangazie, upumzike kwa amani