Friday, December 05, 2014

Kumbukumbu ya kifo miaka 9 ya Mzee Donati Kezirahabi


Kumbukumbu ya kifo miaka 9 ya Mzee Donati Kezirahabi

Ni miaka 9 tangu ulipotangulia katika makazi yako ya milele                                         siku ile ya huzuni 5 Dec 2005.                                                                
Tunakumbuka kwa huzuni upendo na uongozi wako katika familia.  
                Miongozo na mapenzi makubwa uliyotupa ndio yanayotuwezesha kusimama na kumsifu Bwana kila siku. 

Unakumbukwa sana na mke wako Hidaya Kezirahabi,  watoto wako wapenzi na wajukuu, ndugu, jamaa na marafiki wote.

"Bwana akupatie pumziko la milele, na mwanga wa milele akuangazie, upumzike kwa amani."

"Bwana alitoa na bwana alitwaa. Jina lake lihimidiwe milele"