Thursday, December 25, 2014

KAPU LA SIKUU LA 93.7 EFM NI MFANO WA KUIGWA



KAPU LA SIKUU LA 93.7 EFM NI MFANO WA KUIGWA
Mwezi huu wa Disemba 2014,EFM redio ilianza kuwashukuru wasikilizaji wake kwa kuanzisha "Kapu la sikukuu project". Madhumuni ya project hii ni kuwashukuru wasikilizaji wa redio ya 93.7 EFM kwa upendo walio uonyesha tangu kufunguliwa kwa redio hiyo mpaka sasa.

Meneja uhusiano ambae pia ni mmoja wa watangazaji wa kipindi cha Joto La Asubuhi,Kanky Mwaigomole alisema kuwa makapu hayo ya sikukuu yalikua yamejaa hasa vitu vya nyumbani.

"Tumehakikisha ya kwamba kapu hili litakalo muendea mshindi na familia yake,iwe ni furaha tosha kwani kapu mmoja limewekwa nyama,kuku,mafuta ya kupikia,mchele,unga wa ngano na wa sembe,nyanya,vitunguu na kadhalika", alisema Mwaigomole.

 Kanky Mwaigomole alisema kuwa utaratibu wa kushinda kapu hilo wala halikuwa na masharti magumu.

"Tulitumia mziki mfupi bila maneno wa "merry christmas ya jingle bells" na msikilizaji alitakiwa kusikiliza redio yetu mda wote,endapo pale angesikia mwimbo huo wa jingle bells,anaandika ni mda gani umepigwa na ni watangazaji gani waliupiga",alisema.

Kanky aliendelea kusema kwamba kwa yule ambae alipatia jibu ndio alipigiwa simu siku ya leo na kuelekezwa kufwata kapu lake la sikukuu.

Washindi 30 walifanyikiwa kuitwa katika ofisi za EFM na kukabidhiwa makapu yao rasmi siku ya tarehe 24 mwezi wa Disemba 2014.
Mmoja ya washindi wa kapu la sikukuu,Mama Patrick na mwenzake ndani ya Bajaj.

Mshindi wa kapu la sikukuu akipewa kapu lake na Mkuu wa vipindi wa EFM Bwana Dickson Ponella (Dizo one)
Meneja Uhusiano wa EFM,Kanky Mwaigomole,akimsaidia mmoja wa washindi wa Kapu la sikukuu,kuingiza kwenye usafiri.

Mtangazaji wa kipindi cha gurudumu,Swebe,akimsaidia mmoja wa washindi wa kapu la sikukukuu bwana Darisudi wa Bunju.

Bwana Mosheni Mosheni,akiwa na nduguye,walivyokuja kuchukua kapu lao.

Makapu ya kapu sikukuu.