Saturday, December 20, 2014

just in: ajali ya gari mchana huu msitu wa miti wa mafinga, iringa


just in: ajali ya gari mchana huu msitu wa miti wa mafinga, iringa
Wakati Leo Mkoa wa Iringa unaadhimisha wiki ya usalama barabarani yenye kauli mbiu maamuzi yako barabarani ni hatima yetu - fikiri kwanza - Ajali mbaya msitu wa miti wa Mafinga Iringa mcaha huu. Kwa mujibu wa habari zilizotikia aliyepoteza maisha ni Yunith Gwamaka Mwakenja ,majeruhi ni Dereva wa gari hilo ambaye nu mhadhiri wa chuo cha Tumain makumira Tawi la Mbeya Bw Gwamaka Mwakenja  pia  majeruhi mwingine ni Joyce Fredy. Wengine wametibiwa na kuruhusiwa. Chanzo inasadikika kuwa ni mwendo kasi na gari kuacha njia  kwa sababu ambazo bado hazijajulikana na kupinduka.