Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Wilbroad Slaa (katikati) akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kuhusu maazimio ya kikao maalum cha kamati kuu ya chama hicho iliyokutana jana wakati wa kujadili taarifa ya awali ya mchakato wa uchaguzi wa serikali za mitaa na maandalizi ya uchaguzi mkuu ujao jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Mkurugenzi wa Bunge na Uchaguzi, John Mrema na kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA - Bara, John Mnyika.
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) - Bara, John Mnyika akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kuhusu maazimio ya kikao maalum cha kamati kuu ya chama hicho iliyokutana jana wakati wa kujadili taarifa ya awali ya mchakato wa uchaguzi wa serikali za mitaa na maandalizi ya uchaguzi mkuu ujao jijini Dar es Salaam leo.