Friday, December 19, 2014

IKULU YAKANUSHA RAIS KIKWETE KULIHUTUBIA TAIFA LEO



IKULU YAKANUSHA RAIS KIKWETE KULIHUTUBIA TAIFA LEO


Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete
.
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu imekanusha taarifa iliyoandikwa mitandaoni na magazetini kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dk. Jakaya Mrisho Kikwete leo atalihutubia taifa.
Taarifa sahii ni kwamba Rais atalihutubia taifa siku ya Jumatatu, Desemba 22 mwaka huu muda utakaopangwa.