Friday, December 19, 2014

BALOZI KAMALA AKAGUA HOTELI YA NYOTA TANO PATAKAPO FANYIKA KONGAMANO LA BIASHARA MWAKA 2015


BALOZI KAMALA AKAGUA HOTELI YA NYOTA TANO PATAKAPO FANYIKA KONGAMANO LA BIASHARA MWAKA 2015
Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji Dr. Diodorus Buberwa Kamala ( wa tatu kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa taasisi ya Afrika Rise ya Ubeligiji baada ya kukagua Hoteli ya Nyota tano ya Chateau Du Lac patakapo fanyika Kongamano la Biashara na Uwekezaji mwezi Aprili, 2015. Makampuni 500 kutoka Luxembourg, Ufaransa, Canada, Switzerland, Dubai, Ubeligiji, Tanzania, Morocco, DRC na Algeria yanatarajiwa kushiriki. Tanzania imekaribishwa kushiriki katika Kongamano hilo na itapewa fursa ya kutangaza fursa za biashara na uwekezaji zinazopatikana Tanzania. Kongamano hilo litafanyika jijini Genval - Ubelgiji.