Thursday, December 18, 2014

BENKI YA AZANIA TAWI LA MOSHI YAPITA MITAANI NA KUTOA MKONO WA KRISMASI NA HERI YA MWAKA MPYA KWA WATEJA WAKE



BENKI YA AZANIA TAWI LA MOSHI YAPITA MITAANI NA KUTOA MKONO WA KRISMASI NA HERI YA MWAKA MPYA KWA WATEJA WAKE
Mkurugenzi wa Idara ya Oparesheni ya Benki ya Azania, Togolani Mramba (wa pili kushoto), akimkabidhi zawadi mmoja wa wateja wakuu wa Benki hiyo mkoani Kilimanjaro, Mfanyabiashara wa Nafaka, Izina Rashid Msangi, ikiwa ni utaratibu wa kawaida wa Benki hiyo kutoa mkono wa shukrani kwa wateja wake na kuwatakia heri katika sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya, wanaoshuhudia ni wafanyakazi wa Benki hiyo, wakiongozwa na Meneja wa Azania Tawi la Moshi, Bi. Hajira Mmambe.
Timu ya Wafanyakazi wa Benki ya Azania ikipita mitaani kuwazawadia wateja wao na kuwapa mkono wa Heri ya Krismasi na Mwaka Mpya.
Ilikuwa ni msako wa mtaa kwa mtaa, ofisi hadi ofisi, kuhakikisha wateja wote wanapata sababu ya kuendelea kuamini Benki hiyo na kudumisha udugu wa kibiashara.
Mkurugenzi wa Oparesheni wa Benki ya Azania makao makuu, Togolani Mramba (wa kwanza kulia) akiwa na timu ya wataalamu kutoka tawi la Moshi, katika ofisi ya Mfanyabiashara wa Mafuta katika Stendi ya Mboya, Manispaa ya Moshi,  Thomas Siara Mushi (Musisha). 
Bw. Mramba (aliyevaa koti) akimpa mkono wa shukrani na wa kumtakia heri ya Krismasi na Mwaka Mpya, Mfanyabiasha wa Mafuta katika stendi ndogo ya Mboya, Thomas Siara Mushi (Musisha). 
Meneja wa Benki ya Azania Tawi la Moshi, Bi. Hajira Mmambe, akimkabidhi zawadi Mkurugenzi Mtendaji wa Five Star Hardware, Bw. Frank Lesilian, ikiwa ni utaratibu wa kawaida wa Benki hiyo kutoa mkono wa shukrani kwa wateja wake na kuwatakia heri katika sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya.
Ni muda wa kufurahia ushirikiano mzuri katika Biashara na kupongezana. 
Uongozi wa Benki ya Azania Tawi la Moshi, ukiongozwa na Mkurugenzi wa Oparesheni makao makuu, Togolani Mramba ukikabidhi zawadi kwa Mkurugenzi wa Ibra line Company, Ibrahim Shayo kama sehemu ya mkono wa Krismasi na heri ya Mwaka mpya.

 
Hapa kikosi hicho kikakutana na Mkuregenzi Mtendaji wa Dema Construction, Dismas Massawe (aliyeshika mfuko) akikatiza mitaani na kumzawadia akiwa ni mmoja wa wateja wakubwa wa benki ya Azania Tawi la Moshi.
Heka heka za kuwasaka Wateja wakuu wa Benki hiyo mjini Moshi ziliendelea, ambapo safari hii, Kikosi kizima kikiongozwa na Mkurugenzi wa Oparesheni, Togolani Mramba (wa kwanza kushoto), kilibisha hodi katika Ofisi za Mkurugenzi wa Kilimani Pharmacy, Arthur Kiwia na kumpa zawadi yake. 
Safari ikaishia kwa Mmiliki wa Salsalnero Hotel, Benjamin Mengi (ambaye ni mdogo wake na Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Media, Dkt. Reginald Mengi)




Meneja wa Benki ya Azania Tawi la Moshi, Bi. Hajira Mmambe (kulia) akifurahia jambo na Mzee Mengi.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini