Wednesday, December 17, 2014

BALOZI DORA MSECHU AWASILISHA HATI ZAKE ZA UTAMBULISHO KWA RAIS WA ESTONIA,PIA ATEMBELEA CHUO KIKUU CHA Tallinn KUJADILI FURSA ZA MASOMO KWA WANAFUNZI WA TANZANIA

BALOZI DORA MSECHU AWASILISHA HATI ZAKE ZA UTAMBULISHO KWA RAIS WA ESTONIA,PIA ATEMBELEA CHUO KIKUU CHA Tallinn KUJADILI FURSA ZA MASOMO KWA WANAFUNZI WA TANZANIA
Balozi wa Tanzania kwenye Nchi za Nordic na Baltic,Mh. Dora Mmari Msechu (kushoto) akipeana mkono na Rais wa Estonia,Mh. Toomas Hendrik Ilves,wakati alipofika Ikulu ya nchi hiyo kuwasilisha hati utambulisho wake kwa Rais.
Mhe. Balozi Dora Msechu (wa pili kulia) na timu yake wakiwa kwenye Mazungumzo na baadhi ya viongozi wa Chuo  cha Tallinn University of Technology. Mazungumzo yao yalilenga kuanzisha ushirikiano na vyuo vya Tanzania (UDSM na UDOM) na pia kutafuta fursa zaidi za masomo ya sayansi ngazi ya Masters na Phd. Estonia ni moja ya nchi iliyopiga hatua kubwa sana katika masuala ya ICT.