Monday, December 01, 2014

Airtel yakabithi kisima cha maji kwa shule ya msingi Kumbukumbu Dar


Airtel yakabithi kisima cha maji kwa shule ya msingi Kumbukumbu Dar
 Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso (wa pili kulia mbele) na Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Watoto wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Benedict Missani (wa tatu kushoto mbele), wakiwaongoza wafanyakazi wa Airtel Tanzania na wanafunzi kwenye matembezi ya hisani yenye lengo la kuchangisha pesa kiasi cha shilingi milioni 10, kwa ajili ya kuendelea kuboresha Shule ya Msingi Kumbukumbu , yaliyoanzia katika Makao Makuu ya Airtel , Barabara ya Ali Hassan Mwinyi kupitia Bongoyo, Haile Selasie na kuishia shuleni hapo Block 41, jijini Dar es Salaam jana. 
 Wafanyakazi wa Tanzania na wanafunzi wakiwa  kwenye matembezi ya hisani yenye lengo la kuchangisha pesa kiasi cha shilingi milioni 10, kwa ajili ya kuendelea kuboresha Shule ya Msingi Kumbukumbu , yaliyoanzia katika Makao Makuu ya Airtel, Barabara ya Ali Hassan Mwinyi kupitia Bongoyo, Haile Selasie na kuishia shuleni hapo Block 41, jijini Dar es Salaam jana.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso (wa pili kushoto) akimkabidhi Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Watoto wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Benedict Missani, funguo za kisima kipya cha maji safi kilichojengwa  kwa hisani ya Airtel kwa kushirikiana na Wafanyakazi wake,  katika Shule ya Msingi Kumbukumbu, wakati wa hafla iliyofanyika shuleni hapo eneo la Block 41 jijini Dar es Salaam jana. Wanaoshuhudia ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano Malya (kushoto), Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Priscilla Moshi (wa tatu kushoto), na Mwenyekiti wa Shule hiyo, Mwemba Mwilima.
 Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Watoto wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Benedict Missani (kulia) akifungua ili kukagua kisima kipya cha maji safi kilichojengwa  kwa hisani ya Airtel kwa kushirikiana na Wafanyakazi wake,  katika Shule ya Msingi Kumbukumbu, baada ya kukabidhiwa rasmi na Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso (wa pili kushoto), wakati wa hafla iliyofanyika shuleni hapo eneo la Block 41 jijini Dar es Salaam jana. Wanaoshuhudia ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano Malya (kushoto) na Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Priscilla Moshi (wa tatu kushoto).
Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso akifungulia maji ya bomba kama ishara ya uzinduzi rasmi wa  kisima kipya cha maji safi kilichojengwa  kwa hisani ya Airtel kwa kushirikiana na Wafanyakazi wake,  katika Shule ya Msingi Kumbukumbu, wakati wa hafla iliyofanyika shuleni hapo eneo la Block 41 jijini Dar es Salaam jana. Wanaoshuhudia ni Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Watoto wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Benedict Missani (wa tatu kushoto) na Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Priscilla Moshi (wa nne kushoto).