Waziri kiongozi mstaafu Shamsi Vuai Nahodha(kulia)akimkabidhi Mkurugenzi mtendaji wa Vodacom Tanzania Rene Meza, kombe la mshindi wa pili kwa walipa kodi wakubwa nchini wakati wa maadhimisho ya nane ya siku ya mlipa kodi iliyofanyika jijini Dar es Salaam.Vodacom imeongoza katika kundi la sekta ya mawasiliano nchini.
Waziri kiongozi mstaafu Shamsi Vuai Nahodha(wapili kutoka kulia)akiwa katika picha ya pamoja na washindi watatu bora wakubwa walipa kodi kutoka kushoto ni Meneja wa maswala ya kodi wa kampuni ya sigara Tanzania(TCC) Godfrey Ferdinand,wapili ni Mkurugenzi mtendaji wa Vodacom Tanzania Rene Meza,kulia Meneja huduma wa kampuni ya Tanzania Breweries Alois Qande,wakati wa maadhimisho ya nane ya siku ya mlipa kodi iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Waziri kiongozi mstaafu Shamsi Vuai Nahodha(wanne kutoka kushoto waliokaa)akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washindi walipa kodi ambapo Vodacom Tanzania imeongoza katika kundi la sekta ya mawasiliano nchini.
.Wageni mbalimbali waliohudhuria maadhimisho ya nane ya siku ya mlipa kodi nchini iliyofanyika jijini Dar es Salaam,ambapo Vodacom Tanzania imeongoza katika kundi la sekta ya mawasiliano nchini.
Mkurugenzi mtendaji wa Vodacom Tanzania Rene Meza,akiwa ameshikilia kombe la mshindi wa pili kwa walipa kodi wakubwa nchini mara baada ya kukabidhiwa na Waziri kiongozi mstaafu Shamsi Vuai Nahodha(hayupo pichani)wakati wa maadhimisho ya nane ya siku ya mlipa kodi yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.Vodacom imeongoza katika kundi la sekta ya mawasiliano nchini.
Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania imekuwa ya pili kwa kuchangia pato la serikali kupitia kodi ikiwa inaongoza katika kundi la sekta ya mawasiliano.
Akiongea katika kilele cha maadhimisho ya 8 ya Wiki ya Mlipa Kodi yaliyofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere, Mkurugenzi wa Kitengo cha Elimu ya walipa kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania,Richard Kayombo, aliyataja makampuni 3 yanayoongoza kwa kufuata kanuni bora za ulipaji kodi na utunzaji wa kumbukumbu za kulipakodi nchini kuwa ni Kampuni ya Bia Tanzania,Kampuni ya Vodacom na Kampuni ya kutengeneza sigara.
Vodacom Tanzania pia imeongoza katika kundi la walipa kodi wakubwa nchini ikiwa katika nafasi ya pili ikiwa imepiga hatua mbele zaidi ya mwaka jana ambapo ilishika nafasi ya tatu.
Akiongea muda mfupi baada ya kutunukiwa kikombe na cheti ya ushindi kutoka kwa mgeni wa heshima ambaye alikuwa ni Waziri Kiongozi mstaafu wa Zanzibar Shamsi Vuai Nahodha ,Mtendaji Mkuu wa Vodacom Rene Meza alisema "Napenda kuwashukuru wafanyakazi wote wa Vodacom na wateja wetu wote ambao wanaendelea kutuweka mbele kwa ushirikiano wao na kutuamini ambapo tumeweza kuwa wachangiaji wakubwa
Alisema kitendo cha Mamlaka ya MapatoTanzania (TRA) kutambua kwa mara ya pili nafasi ya Vodacom katika kulipa kodi za serikali kinathibitisha dhamira ya kweli ya kampuni kuwa ni mwekezaji makini ambaye uwekezaji wake na uchangiaji wake mapato ya serikali umekuwa ukikua mwaka hadi mwaka.Meza alisema mpaka sasa Vodacom imewekeza nchini zaidi ya shilingi trioni 1.7/- na bado ina dhamira ya kuendelea kuwekeza na kukuza sekta ya mawasiliano nchini.
Kuhusu ni kiasi gani cha kodi ambayo kampuni imelipa mwaka huu alisema "katika kipindi cha miezi sita cha mwaka wetu wa fedha kuanzia mwezi Aprili mpaka Septemba 2014,tumelipa kodi serikalini shilingi 27.6 bilioni/- kwa Kodi ya mapato,na tulikusanya shilingi bilioni 141.5 kwa kodi ya Ongezeko la Thamani na kodi ya zuio kwa niaba ya serikali".
Pia aliongeza kuwa mwaka jana Vodacom ililipa kodi ya shilingi 47.1 bilioni/-kwa kodi ya mapato pia ilikusanya zaidi ya shilingi bilioni 262.8 za kodi ya ongezeko la thamani ,kodi ya zuio na kodi nyinginezo zinazolipa serikalini. "Tunatimiza taratibu za kulipa kodi kulingana na sheria za serikali na kuendelea kutimiza matakwa ya serikali.Ushindi huu tulioupata kwa mara ya pili ni uthibitisho wa kutosha".Alisema.
Kuhusu malengo ya Kampuni katika kipindi cha miezi ichache ijayo,Meza alisema itaendelea kutekeleza majukumu kwa wadau wake wote.Vodacom inaongoza kwa mtandao mpana na ubunifu wa kiteknolojia nchini ambapo hivi sasa mtandao wake umewafikia asilimia 90 ya watanzania pia inatoa huduma ya internet ya 3G nayo imesambaa nchini kote na kuwawezesha watanzania wengi kupata huduma ya internet kwa urahisi na kwa gharama nafuu.Vilevile kampuni imebuni huduma mballimbali za kibenki,usomaji kwa njia ya mtandao,biashara,kilimo,afya,usalama na inaendelea kubuni huduuma nyinginezo za kufanya maisha ya watanzania kuwa murua.