Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Spika wa Bunge, Anne Makinda kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Novemba 7, 2014 katika tafrija ya kumpongeza Spika kwa kuteuliwa kuwa Rais wa Mabunge ya SADEC iliyofanyika mjini Dodoma. Kulia ni Mbunge wa Viti Maalum Anna Abdallah na watatu kulia ni Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Angela Kairuki.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Spika wa Bunge, Anne Makinda kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Novemba 7, 2014 katika tafrija ya kumpongeza Spika kwa kuteuliwa kuwa Rais wa Mabunge ya SADEC . Kulia ni Mbunge wa Viti Maalum Anna Abdallah na wapil kulia ni Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Angela Kairuki na kushoto ni Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Dr. Pindi Chana.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Spika wa Bunge Anne Makinda (kushoto) wakimsikiliza Naibu Waziri wa katiba na Sheria, Angela Kairuki (katikati) alipotoa maelezo kuhusu zawadi ya picha ambayo wabunge walimzawadia Spika Makinda katika tafrija ya kumpongeza kwa kuteuliwa kuwa spika wa Mabunge ya SADEC iliyofanyia kwenye viwanja vya Bunge mjioni Dodoma Novemba 7, 2014.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiongozana na Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu (kushoto) na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Aggrey Mwanri baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Arusha ambako alifunga Mkutano wa kupiga vita ujangili wa wanayamapori na kuendeleza uhifadhi wa wanayamapori uliofanyika mjini Arusha Novemba 8, 2014.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu (wapili kushoto) na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Aggrey Mwanri (kulia) baada ya kufunga Mkutano wa kupiga vita ujangili wa wanayamapori na kuendeleza uhifadhi wa wanayamapori mjini Arusha Novemba 8, 2014. Kushoto ni Mbunge wa Kahama, James Lembeli.Wapili kulia ni Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki, Dkt Richard Sezibara.Picha na ofisi ya Waziri Mkuu